The House of Favourite Newspapers

Abdul Kambaya Afunguka Sababu za yeye kujiunga na Chama cha Mapinduzi – Video

MWANASIASA maarufu nchini Abdul Kambaya

MWANASIASA maarufu nchini Abdul Kambaya leo Julai 19, 2024 amefunguka kupitia kipindi cha Front Page ya kinachoruka kupitia Global Radio na Global TV Online sababu za yeye kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) akijiondoa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .

Kambaya alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) na wengine zaidi ya mia tano (500), mnamo Julai 17, 2024 katika mkutano mkuu wa hadhara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla uliofanyika kqtika Uwanja wa Mwinyijuma Jijinj Dar es salaam.

Kabla ya kujiunga na CCM, Kambaya alikuwa mwanachama wa chama cha Chadema.