The House of Favourite Newspapers

Acacia Stand United kuja kivingine

0

Stand United

Kikosi cha Acacia Stand United.

Na Johnson James, Mwanza
BAADA ya kuwa kwenye mgogoro wa kiuongozi kwa muda mrefu, timu ya Acacia Stand United kupitia kwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi, Muhibu Kanu imesema kuwa migogoro hiyo imekwisha hivyo mipango yao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa timu inamaliza ndani ya nafasi tano za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Stand United ambayo kwa sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig iliingia kwenye mgogoro wa kiuongozi baada ya kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kutoa udhamini wa shilingi bilioni 2.5 kwa mkataba wa miaka miwili ambapo baadhi ya viongozi wa mkoa wa Shinyanga walitaka kuwa viongozi lakini baadaye wakaamuliwa waiache timu hiyo mikononi mwa viongozi waliotangulia.

Akizungumza na tovuti hii, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi wa Acacia Stand United Muhibu Kanu amesema kuwa kwa sasa migogoro hiyo imeshamalizika tangu waziri mwenye dhamana na michezo Nape Nnauye kuitaka kamati ya mkuu wa mkoa kurudisha madaraka kwa viongozi waliokuwepo tangu awali.

“Kwa sasa hali ndani ya timu ni shwari na mipango yetu ni kuhakikisha kuwa timu inaendelea kufanya vizuri kwenye ligi ” alisema

Aidha Kanu amewaomba wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuhakikisha kuwa wanendelea kutoa sapoti ya kutosha kwa timu hiyo maana ni timu ya wapiga debe wa stendi.

“Timu yetu mashabiki wake wakubwa ni wapiga debe wa Shinyanga hivyo tunaomba waendelee kutuunga mkono kwani timu sasa iko katika hali ya ushindani“ alisema Kanu.

Leave A Reply