Achana na Mondi… Mbosso Aweka Rekodi ya Watoto

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa! Ukimwacha Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, staa mwingine wa lebo hiyo, Mbwana Yusuf Kilungi ‘Mbosso’ ameweka rekodi ya kuwa na idadi kubwa ya watoto.

 

Ukimwacha Diamond au Mondi ambaye ana watoto watatu huku akitarajia kupata wa nne kutoka kwa wanawake watatu tofauti, wikiendi iliyopita Mbosso naye alipata mtoto wa tatu.

 

Mbosso na mwanadada maarufu mjini, Rukia Rucky wamejaliwa kupata mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la Khan Junior. Mbosso amekuwa akijiita Mbosso Khan, jina la mwigizaji mkubwa wa filamu za Kihindi.

 

Mbosso alikiri kwa gazeti hili kuwa huyo ni mtoto wake wa tatu kutoka kwa Rukia.

“Ni kweli kwa sasa nina watoto watatu na ninaishi nao vizuri tu,” alisema Mbosso mwenye umri wa miaka 28.

 

Kama ilivyo kwa bosi wake Mondi, Mbosso naye amepata watoto hao kutoka kwa wanawake watatu tofauti.

Kitu kingine ambacho Mbosso ameweka rekodi kwenye lebo hiyo, ni kitendo cha kupata watoto hao wote wa kiume, tofauti na Mondi ambaye kati ya wanaye watatu, mmoja ni wa kike, Tiffah Dangote.

 

Kwa mujibu wa Mbosso, watoto wawili wa awali walizaliwa na mama tofauti, lakini ndani ya mwezi mmoja hivyo baadhi ya watu kuamini ni mapacha.

Jambo lingine ni kwamba, sasa Mbosso amezaa na wanawake wawili nchini Tanzania na mmoja nchini Kenya.

 

Hata hivyo, wanawake aliozaa nao mwanzo hakudumu nao kwani mapenzi yaliisha na kila mmoja kuchukua hamsini zake, lakini Mbosso akabaki na jukumu la kulea wanaye.

Baadhi ya mastaa wengine wenye watoto wengi kutoka kwa mama tofauti ni pamoja na Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

 STORI: NEEMA ADRIAN, DAR


Loading...

Toa comment