The House of Favourite Newspapers

Acheni Yanga iitwe Yanga, Yaipiga Prisons 2-1 Uhuru

YANGA inazidi kutusua kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya jana Alhamisi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana.

 

Katika mchezo, Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kujipatia bao kupitia kwa kiungo wake wa kimataifa raia wa DR Congo, Papy Kabamba Tshishimbi dakika ya 23 akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo uliopigwa na Ibrahim Ajibu ambaye kwa sasa amefi kisha asisti 17 msimu huu katika ligi hiyo.

 

Bao hilo lilidumu kwa dakika tisa pekee, kwani dakika ya 32, Ismail Kada aliisawazishia Prisons akitumia makosa ya walinzi wa Yanga walioshindwa kuondoa hatari langoni mwao kutokana na mpira wa kona uliopigwa na Salum Kimenya.

 

Kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambacho Yanga ilipiga jumla ya mashuti mawili pekee huku Prisons ikipiga manne, kilishuhudiwa matokeo yakiwa sare ya bao 1-1 jambo ambalo lilimkasirisha zaidi Kocha wa
Yanga, Mwinyi Zahera.

 

Kipindi cha pili Yanga ilionekana kuwa na hasira ya kuibuka na ushindi kutokana na kucheza nyumbani, ambapo ilifanya mabadiliko ya wachezaji watatu.

 

Alitoka Ajibu akaingia Deus Kaseke, Jaff ary Mohammed nafasi yake ilichukuliwa na Haji Mwinyi na Mohammed Issa alimpisha Said Juma Makapu.

 

Mabadiliko hayo yaliyofanyika kwa nyakati tofauti, kwa kiasi kikubwa yalizaa matunda kwani dakika ya 66, Heritier Makambo aliifungia Yanga bao la pili na la ushindi katika mchezo huo.

 

Baada ya kufunga bao hilo Acheni Yanga iitwe Yanga huku akiwa na furaha ya kufi kisha mabao 16, Makambo aliwachukua wenzake na kwenda kushangilia kwa staili ya kupiga ‘selfi e’ wakitumia simu ya mmoja wa wapiga picha uwanjani hapo.

 

Ushindi huo umeifanya Yanga kufi kisha alama 80 kileleni na kuiacha Simba ikibaki na alama zake 72 katika nafasi ya pili. Yanga imeizidi Simba kwa michezo sita.

 

Ilishuhudiwa kwenye mchezo huo Kocha Msaidizi wa Simba, Denis Kitambi akiwa makini kuwachunguza Prisons ambao Jumapili hii watapambana kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya ukiwa ni mwendelezo wa ligi hiyo.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.