The House of Favourite Newspapers

ACHILIA ISHU YA MO, MASTAA HAWA NAO… WALITEKWA, WAKAZUA GUMZO!

Mohammed Dewji ‘Mo’

WIKI mbili zilizopita kila kona kulikuwa na sintofahamu baada ya kutokea tukio la kutekwa kwa bilionea namba moja nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’. 

Mo alitekwa alfajiri ya Oktoba 11, mwaka huu na watu wasiojulikana nje ya Hoteli ya Colosseum alipokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi kwenye gym iliyopo ndani ya hoteli hiyo.

 

Japokuwa Mo alipatikana salama usiku wa kuamkia Oktoba, 19 baada ya kutupwa na watekaji hao katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar lakini sakata lake lilikuwa gumzo  kwa kuripotiwa na vyombo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

 

Ukiachilia mbali hilo, wapo mastaa ambao nao walipitia katika sakata la kutekwa na kuachiwa wakiwa salama na wengine wakiwa wamefariki dunia. Star Showbiz linakuanikia baadhi tu ya mastaa hao;

Related image

Kim Kardashian

Mwanamama huyu ambaye ni mke halali wa rapa Kanye West akiwa amezaa naye watoto watatu naye alikumbwa na tukio la kutekwa. Sakata hilo lilitokea Oktoba 2, 2016 ambapo Kim alikwenda Paris, Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria maonesho ya mavazi. Usiku akiwa ndani ya hoteli moja ya kifahari katika jiji hilo, ghafla alivamiwa na wanaume wawili waliokuwa wamevalia sare za polisi.

 

Wanaume hao waliingia chumbani kwake na kumfunga mikono na miguu kisha kumfungia kwenye bafu na baada ya hapo walitoroka na vito vya thamani ya dola milioni 10.5 (zaidi ya bilioni 22 za Kibongo). Hata hivyo, baada ya saa kadhaa Kim alikuja kuokolewa na polisi ambapo baada ya kipindi kifupi walifanikiwa kuwakamata wahusika wa tukio hilo na kuwachu-kulia hatua.

Image result for Alex Band

Alex Band

Staa huyu wa Calling Band iliyotikisa mwanzoni mwa miaka ya 2000 naye anaingia katika listi hii ya kukumbwa na sakata la kutekwa. Alex alitekwa 2013 alipokuwa ameenda na wenzake eneo la Michigan, Marekani kwa ajili ya kufanya tamasha kubwa la kurudisha uhai wa kundi lao.

 

Kama ilivyo kwa Kim, Alex naye alikumbwa na kasumba hiyo ambapo watekaji walimuwekea bastola na kumtaka atoe pesa. Licha ya kuwa mbishi, watekaji hao walimpiga vibaya eneo la pua na kumtoa meno kadhaa kisha kumtupia katika njia ya reli.

Image result for Veruska Ramirez

Veruska Ramirez

Ni Miss Venezuela 1997 ambaye pia ni Miss Universe 1998 ambapo naye ameingia katika listi ya waliowahi kutekwa na kuzua gumzo. Mwaka 2003, Veruska alitekwa kwa saa tatu. Watekaji hawakutaka kumdhuru bali walihitaji asaini boksi lililojaa kalenda walizokuwa wameziandaa zikimuonesha Veruska akiwa mtupu. Watekaji walimtaka asaini kila kalenda yenye picha yake ya utupu na baada ya hapo walimuachia kisha wakazisambaza kalenda hizo mitaaani.

Image result for Meenakshi Thapa

Meenakshi Thapa

Ni staa wa filamu kutoka Bollywood mwenye filamu kadhaa ikiwemo ya kutisha iitwayo 404. Aprili 2012, Meenakshi akiwa katika maandalizi ya muvi mpya, alitekwa na watu wawili ambao pia ni wapenzi, Amit Jailswal na Preeti Surin waliokuwa wakitengeneza muvi pamoja. Baada ya kutekwa, vijana hao waliwasiliana na familia ya Meenashi na kuitaka kutoa rupee 1,500,000 (zaidi ya milioni 46) la sivyo wangemchezesha filamu ya ngono kwa lazima.

 

Mama wa Meenakshi hakuwa na uwezo, aliwatumia watekaji kiasi cha rupee 60,000 (zaidi ya milioni 1.8) kupitia akaunti ya benki ya mwanaye huyo ili wazitoe. Kiasi hicho kidogo cha pesa, kilifanya watekaji wamuue Meenakshi na kiwiliwili chake kukitupa ndani ya tenki la maji huku kichwa kikipatikana njia ya basi iendayo Mumbai. Hata hivyo, watekaji hao walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha.

Comments are closed.