The House of Favourite Newspapers

Video: ACT Waitaka Serikali Ieleze Ukweli Nchi Imekumbwa na Njaa, Walalamika Kuchezewa Faulo Uchaguzi Mdogo

dsc_0141

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT (katikati), akizungumza na waandishi wa habari.  Kulia ni Ester Kyamba, katibu wa Ngome ya Wanawake Taifa na John Patric Mbozu, Kaimu Katibu wa Mafunzo na Uchaguzi.

dsc_0139Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo, leo.

dsc_0142

 

dsc_0143 dsc_0144 dsc_0145 dsc_0146 dsc_0150 dsc_0151

Chama cha ACT Maendeleo kimelalamika kuwa kinachezewa rafu na baadhi ya watendaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwenye Kata ya Nkome ili kuhakikisha kwamba Chama Cha Mapinduzi kinapata ushindi katika uchaguzi wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Makao Makuu ya ACT Wazalendo, Kijitonyama jijini Dar, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu alidai kuwa wazee walikusanywa na kuahidiwa kupatiwa matibabu bure na wakati wa kwenda kwenye kikao hicho walitakiwa kwenda na vitambulisho vyao vya kupigia kura.

“Wale ambao hawakuwa na vitambulivyo waliambiwa waende wakatafute hata vya ndugu zao… huu ni mpango wa kukibeba chama tawala. Maswali ya msingi ya kujiuliza ni kuwa kwa nini zoezi hilo lianze katika kipindi hiki cha kampeni? Kwa nini wazee hao walazimishwe kwenda na vitambulivyo vyao vya kupigia kura?” alihoji Shaibu.

Alisema wameiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulalamikia vitendo hivyo, wakati huo akaongeza kuwa kuhusu njaa nchini, aliitaka serikali kuwajibika kuwahudumia wenye njaa kwa kuwa tatizo hilo limetokana na ukame sehemu husika na wala siyo uzembe.

Elvan Stambuli na Denis Mtima/ GPL

ACT Yadai Kuhujumiwa Chaguzi Ndogo

Comments are closed.