ACT Wazalendo Kukutana na Wanahabari

zitto-kabwe

Chama cha Alliance for Change Tanzania (ACT- Wazalendo), Alhamisi ya Januari 12, 2017, kitafanya mkutano na waandishi wa habari, kuzungumzia mambo mbalimbali ya kitaifa, pamoja na kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa habari wa chama hicho, Abdallah Khamis, mkutano huo utafanyika makao makuu ya chama hicho, Sayansi, Kijitonyama jirani na Kanisa la KKKT, kuanzia saa 4:30 asubuhi.

Taarifa zaidi kuhusu mkutano huo, zitakujia kupitia mtandao huu.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment