The House of Favourite Newspapers

ACT Wazalendo wazungumzia utafiti wa Twaweza

0

Kutoka kushoto ni,Mjumbe wa Chama Cha ACT Wazalendo,Emmanuel Mvula, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa, Nixon Tugara na Mkurugenzi wa Kampeni za uchaguzi Taifa, Venance Msebo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa, Nixon Tugara (katikati) akisoma taarifa yake.

Wanahabari wakichukua tukio.

CHAMA cha Act- Wazalendo hii leo kimezungumzia utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza juu ya mgombea urais kupitia chama hicho, Anna Mghwila uliotolewa jana na viongozi wa taasisi hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni Taifa, Nixon Tugara amesema kuwa chama cha ACT Wazalendo kimeyapokea matokeo hayo ya awali na kuyapitia kwa kina juu ya tafiti na maoni ya wananchi kuhusu siasa uliofanywa na taasisi ya Twaweza.

Amesema kuwa licha ya kuonesha hali hiyo ya utafiti wao wamefarijika kwamba chama chao ni chama pekee nje ya CCM na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kilichotajwa na wapiga kura zaidi ya asilimia moja, hivyo ikidai chama chao kimekuwa cha nne katika kukubalika kwa wapiga kura nyuma ya vyama vingine.

Aliongeza kuwa wanazidi kufarijika kwamba watafiti wamekiri wazi kuwa takwimu za utafiti zilikusanywa katika kipindi ambacho chama chao cha ACT Wazalendo kilikuwa hakijamtangaza mgombea wake wa urais na pia wakati huo walikuwa bado hawajatangaza wagombea wao kupitia ubunge wala kuzindua kampeni.

Aidha aliongeza kutokana na kufanya vizuri katika uzinduzi wa kampeni zao na bidii kubwa ambayo mgombea wao mama Anna Mghwira na wagombea wa ubunge na udiwani wamekuwa wakifanya katika kampeni zinazoendelea nchi nzima, hivyo ni imani yao kama utafiti ungefanyika leo kuwa wangefanya vizuri zaidi.

”Ninachowaomba wagombea wetu na wanachama, wapenzi wa ACT Wazalendo pamoja na viongozi wa chama wachukulie matokeo haya ya utafiti kama changamoto ya kuongeza bidii katika kampeni zetu,” alisema Tugara.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

 

Leave A Reply