ACT Wazalendo Yamzawadia Gari Mwenyekiti Mstaafu wao Juma Duni Haji – Video
CHAMA cha ACT Wazalendo Septemba 4, 2024 kimemkabidhi gari aina ya Prado Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho, Juma Duni Haji ikiwa ni sehemu ya kutekeleza Sera ya Chama hicho ya kuwaenzi Viongozi Wastaafu.
Babu Duni pia amezawadiwa pia zawadi mbalimbali na Viongozi wa Kitaifa, Mikoa na Majimbo, hafla hiyo ya kumkabidhi gari imefanyika Visiwani Zanzibar ambapo ACT imeanza kutimiza sera mpya ya Chama ya kuwaenzi Wastaafu na kuanzia leo wamemuenzi Duni Haji kwa kazi zake alizofanya tangu mwaka 1992 mpaka leo.
Viongozi mbalimbali wa ACT Wazalendo wamehudhuria ikiwemo Kiongozi wa Chama Doroth Semu, Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Otham Masoud Othman , Makamu wenyeviti wa Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Mkuu pamoja na mamia ya Wanachama wa ACT Wazalendo.