Adaiwa Kunywa Energy Drink na Nguvu Zake za Kiume Zaongezeka Ghafla

 

SHIRIKA la kupima viwango vya ubora wa bidhaa nchini Uganda, The Uganda National Bureau of Standards (UNBS), linatarajiwa kufanya utafiti na vipimo zaidi kuhusu ubora wa kinywaji cha Natural Power SX, kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini kinachodaiwa kuwa na dawa ya Viagra.

 

Kulingana na gazeti la The Sunday Monitor nchini Uganda vipimo vya maabara vilivyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti Matumizi ya Dawa nchini Uganda (NDA) vilibaini kwamba kinywaji cha Natural Power SX kina Sildenafil Citrate, ambayo hukuzwa kama Viagra.

 

The Sunday Monitor linasema kuwa NDA mnamo Desemba 28 kupitia barua iliotiwa saini na  David Nahamya kwa niaba ya katibu wa mamlaka hiyo, Bi Dona Kusemererwa, liliripoti kwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la ubora wa bidhaa nchini Uganda Dkt. Ben Manyindo kwamba mlalamishi alidai kwamba baada ya kutumia kinywaji hicho nguvu zake za kiume ziliongezeka kwa muda mrefu mbali na kiwango cha mapigo ya moyo pamoja na kutokwa na jasho isivyo kawaida.

 

Kufuatia malalamiko hayo mamlaka ilichukua sampuli ya bidhaa hiyo na kuichunguza.

 

Kwa mujibu wa gazeti hilo matokeo yake yalionyesha kuwa bidhaa hiyo ya Slidenafil Citrate iliwekwa katika kinywaji hicho kulingana na barua hiyo.

 

Slidenafil  inayouzwa kwa jina maarufu kama Viagra ni dawa inayotumika kutibu matatizo ya nguvu za kiume pamoja na tatizo la shinikizo la damu. Hutumika kwa kula ama kudungwa moja kwa moja katika mishipa ya damu

 

Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Monitor kisa hicho kinajiri wakati ambapo mamlaka ya NDA inayosimamia dawa nchini Uganda mwezi uliopita ilionya kwamba dawa ya Viagra ilipatikana imechanganywa katika dawa za miti shamba.

 

Vyombo vya habari vilinukuu mamlaka ya NDA ikisema kwamba asilimia 55.08 ya dawa za mitishamba pamoja na dawa za vyakula tofauti zimechanganywa na Sldenafil pamoja na dawa nyengine hatari.

 

Suala hilo liliwasilishwa kwa shirika la ubora wa bidhaa na mamlaka ya kudhibiti utumizi wa dawa ambao wanasema kuwa walipata sampuli za Natural Power SX ambazo zilikuwa zimetiwa dawa ya Viagra baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mteja aliyekuwa na wasiwasi.

 

Kinywaji hicho hutengezwa nchini Zambia.

 

Kwa mujibu wa gazeti la the Sunday Monitor, mlalamikaji, kulingana na NDA, alikabiliwa na ongezeko la nguvu za kiume kwa takriban saa sita mbali na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida baada ya kunywa kinywaji hicho.

 

Godwin Muhwezi mkuu wa idara ya uhusiano mwema aliambia gazeti la Jumapili la The Monitor kwamba kundi la wataalam watachunguza madai ya barua hiyo kutoka NDA na kutoa mipango ya kupima zaidi bidhaa hiyo.

 

”Nitafanya majadiliano zaidi kabla ya kuthibitisha kwenu ni hatua gani tutakayochukua. lakini kile ambacho tutahitajika kufanya ni kuchunguza yaliyomo katika barua ili kwenda kuchukua vipimo kwa uchunguzi zaidi.”

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART ONE)

Loading...

Toa comment