The House of Favourite Newspapers

Adam Adam, Metacha Ndani ya Polisi Tanzania

0

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Al Wahda FC ya nchini Libya, Adam Adam amefanikiwa kujiunga na Polisi Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Adam kabla ya kujiunga na Polisi Tanzania alikuwa anakipiga katika Klabu ya Al Wahda FC ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Tanzania.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa timu hiyo, Juma Hassan amethibitisha kuwa ni kweli wamewasajili wachezaji hao ili kuweza kuongeza nguvu katika kikosi chao cha msimu ujao.

Aliongeza kuwa, katika kikosi chao zilibaki nafasi mbili lakini moja tayari imepata mwenyewe ambaye ni kipa Metacha Mnata aliyekuwa anachezea Yanga katika msimu uliopita na taarifa za usajili wake wote utajulikana rasmi leo na watamtangaza rasmi.

 

“Malengo yetu kama timu ni kufanya usajili mzuri kwa ajili ya msimu ujao na ndio maana tumewasajili wachezaji hao na wengine ambao tumewasajili kutokana na uhitaji wa timu.

 

“Tumemsajili Adam kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongeza nguvu katika kikosi chetu cha msimu ujao lakini pia Metacha ambaye tutamtangaza kesho (leo) pamoja na wachezaji wetu wote wapya.”

STORI NA Richard Ngailla – GPL


Leave A Reply