Adel Zrane Afariki Duniani Ghafla mchana wa leo Rwanda
Kocha wa viungo aliyewahi kuitumikia Klabu ya Simba kuanzia 2018 mpaka mwaka 2021 alipoondoka, Adel Zrane amefariki duniani ghafla mchana wa leo, April 2, 2023.
Mpaka anafikwa na mauti, Zrane alikuwa kocha wa viungo wa APR FC ya nchini Rwanda.
Taarifa ya APR FC imeeleza kuwa chanzo cha kifo chake bado haijafahamika.
Akiwa Simba, Zrane aliwahi kufanya kazi na makocha kadhaa akiwemo Patrick Aussems, Sven Vandebroeck na Didier Gomes ambapo alikuwa kipenzi cha mashabiki kwa namna alivyowafanya wachezaji kuwa imara kimazoezi.