The House of Favourite Newspapers

Adhabu chungu, ya kijasiri kwa mpenzi aliyekusaliti

0

unhappy-couple-on-valentines-dayNi wiki nyingine tunakutana tena kupitia safu hii ambayo kimsingi tunakumbushana na kuelimishana juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi. Naamini wewe msomaji wangu umzima bukheri wa afya na uko tayari kabisa kupitishia macho kile ambacho nimekuandalia kwa siku hii ya leo.

Mpenzi msomaji, hakuna kitu kinachouma katika uhusiano wa kimapenzi kama kusalitiwa kiasi cha baada kufikia hatua ya kujiua ama kuwa vichaa wanapokumbana na tatizo hilo.

Kwa wanaume, wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao wanawasaliti wamekuwa na kasumba ya kutunisha misuli na kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa nao kisha kuwaacha wapenzi wao. Hili limebainika si jambo sahihi hasa linapotokea kwa watu wawili waliotokea kupendana.

Kuna wengi ambao waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi, lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa dharau na kejeli huku wakibembelezana.

Kama nilivyosema awali, usaliti ni jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Hakuna suala la kuazima mke katika maisha, watu huazimana magari na pesa lakini mpenzi, hakuna jasiri wa namna hiyo! Huo ndiyo ukweli wenyewe lakini, kupiga au kuacha unapobaini mpenzi wako amekusaliti kunasaidia?

Jibu la kitaalumu ambalo naamini kuna wanaoweza kulikataa ni kwamba hakusaidii. Hakusaidii kwa sababu, ukimpiga hiyo ni adhabu inayoishia hapo hapo, kesho wanakutana, wanakusaliti tena kupozana machungu.

Ukimwacha utakutana nao mitaani wakiwa wameshikana mikono kwa uhuru na raha zao, wewe utaumia sana moyoni mwako. Ukiwaua na wewe utauawa, huku wanadamu wenzako wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri.

Jamani usaliti upo si tunawaona wake na wapenzi wa watu wanaingizana gesti kila siku?
Hivyo basi, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku utakutana na meseji kali za kimahaba zikitoka ama kwenda kwa mwanaume mwingine. Utafanyaje baada ya kubaini hivyo?

Maana kama ni tukio basi utakuwa umelishuhudia laivu bila chenga. Wiki hii nataka kutumia safu hii kuwaelimisha wanaume wenzangu adhabu sahihi ya kumpa mpenzi wako pale utakapomfumania ama utakapobaini anakusaliti kwa namna moja ama nyingine.

Wanaume katika suala hili wanatakiwa kuweka kando mambo ya mabavu. Ndiyo maana leo nasema hivi, ukimfumania mpenzi au mkeo, fuata hatua hizi nne katika kukabiliana na tatizo hilo bila madhara. Kwanza piga moyo konde, pili ondoka eneo hilo tena kwa kukimbia. Ukifika nyumbani, endelea kunywa maji ili kupoza presha.

Akirudi mpenzi wako jitahidi kumkaribisha kwa mahaba na usimuulize ulichoona.
Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza ni hatua gani unafikiria kumchukulia.

Na kwa yule uliyemshika naye, vivyo hivyo usizozane naye, mwache!
Utashangaa anahama eneo maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora kumbe umeamua kujituliza tu!

Wanasaikolojia wamethibitisa adhabu hii kuwa ina uchungu kuliko kupiga au kukemea licha ya kwamba inahitaji ujasiri wa hali ya juu.

Leave A Reply