The House of Favourite Newspapers

Aeleza alivyomjua Godfather kupitia Google

0

AY

Ambwene Yessaya”AY”

BAADA ya wiki iliyopita AY kusimulia jinsi alivyosafiri kwa basi kwenda nchini Uganda wakati huo akiwa hana ndugu, rafiki wala jamaa na alikuwa hajawahi kufika huko lakini alipofika alipata bahati ya kupokelewa na kijana mmoja wa Kitanzania aliyekuwa akifahamiana na Bobi Wine.
Pia alieleza jinsi anavyopanga kazi zake kwa hatua na mikakati aliyonayo kutambulika dunia nzima.
Songa naye mwenyewe…

“Kuna siri nilikuwa sijawahi kuwapa hasa kuhusiana na suala zima la video zenye ubora ambazo mataifa mengi hususan Nigeria wamekuwa wakifanikiwa kwa hilo.
“Kuna kipindi nilifikiria na kuona kwa nini sisi (Watanzania) tunashindwa kwenda sawa na video kama za Nigeria ndipo nilipopata wazo la kubanana nao hawa watu ili kubaini wanafanya kazi na nani na kama wanafanya kazi na huyo mtu iwe tunapishana lugha tu lakini ubora tuko sawa.

“Niliamua kutumia intaneti kujua ni waongozaji gani wanaofanya video za wasanii wa Nigeria, nikaingia moja kwa moja kwenye mtandao unaoitwa Google na kuandika Do Me, P-Square directed by ikadondoka jina Godfather sababu video zake zilikuwa zinaandikwa Jude Okoye (kaka wa P Square) na zilikuwa haziandikwi Godfather.

“Kwa hiyo nikaangalia pale nikaona ndiyo huyu, nikatafuta website ya Godfather ikaja nikakuta ameweka video zake nyingi alizozifanya.Nikatafuta eneo la mawasiliano kisha nikampigia simu.godfazaa

Godfather

“Nilipojitambulisha, napenda nifanye naye kazi, akanipangia bei, nakumbuka ilikuwa kama dola elfu 20. (zaidi ya milioni 40 za Kitanzania) nikaona sasa mbona pesa nyingi endapo nitamtumia kwa njia ya Western Union.
“Kwa bahati nzuri Godfather alikuwa na safari ya Nairobi alikoenda kufanya matangazo hivyo tukakubaliana tukutane huko kulipana na kuzungumza zaidi.”
AY anasema walikutana Nairobi na kukabidhiana fedha hizo kisha kupanga tarehe ya kufanya video lakini wakati wanakabiadhana, Godfather alimshauri waandikishane kwanza japo AY alisema anamuamini na hakukuwa na haja ya kufanya hivyo mwishowe wakakubaliana japo wapige picha kama ushahidi.

“Pamoja na kulipa fedha hiyo yote, ratiba ya Godfather ilikuwa bado imebana kwa kuwa P-Square walikuwa wamebook siku 10 za kufanya naye kazi Afrika Kusini. Godfather aliniuliza kama nafahamiana na P-Square na kunitaka niwaombe kama wanaweza kunipa siku mbili kati ya kumi walizochukua, nikafanya hivyo wakakubali.
“Nikamchukua mwanangu Marco Chali, nikamuambia Marco hivyohivyo na passport yako tutanunua nguo hukohuko. Ndiyo hivyo tukafanya Party Zone na ulikuwa ni uzoefu mkubwa. Kikubwa zaidi mimi na Marco ndiyo ulikuwa mradi wetu wa kwanza.

“Kikubwa ninachoweza kumalizia kwa vijana wenzangu ni kujituma katika kazi wanazozifanya, haijalishi wanafanya kazi gani. Mimi baada ya kumjua Godfather niliamua kumtafuta muongozaji mwingine aliyetengeneza Zigo (remix) anaitwa Alessio Bettochi ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Studio Space Pictures (SSP), ambao pia wamefanya video mpya ya MwanaFA ‘Asanteni Kwa Kuja’. Nilikuwa sijawahi kukutana na Alessio mwanzo kabla ya kufanya hii Zigo na kitu kikubwa ambacho nilichokuwa nakiangalia, ilikuwa ni mazingira kuwa nimeshafanya video na Godfather, nimei-brand hiyo lebo yake na kweli imekubalika, sasa nashukuru na kwa upande wa Alessio wameanza kumuelewa.
“Mwisho kabisa mwaka huu, nawaahidi kuwa nitahakikisha natoa nyimbo tano kama siyo sita ili kufidia madeni ya miaka iliyopita ambayo sikutoa nyimbo nyingi. Niwatakie kazi njema na asanteni kwa kuisoma simulizi hii kwani naamini wengi mmejifunza na kutamani kufuata nyayo zangu,” alimalizia AY.

MWISHO.
Baada ya kumalizika kwa simulizi ya AY, jiandae kusoma inayohusu maisha ya mchekeshaji maarufu kutoka Kundi la Mizengwe, Mkwere.

Leave A Reply