The House of Favourite Newspapers

Afa kwa Kipigo, Ndugu Wasusia Maiti Kituo cha Polisi – Video

0

Maisha ya Akilwa Emanuel Mbise, mlinzi wa kampuni binafsi ya Speed Security Guard iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam, yamekatishwa kikatili baada ya kile ambacho ndugu wanadai kuwa ni kupigwa vibaya na askari wa Kituo cha Polisi Urafiki mpaka kufikia hatua ya kulazwa akiwa mahututi na hatimaye kupoteza maisha usiku wa Oktoba 30, 2021!

 

Waandishi wetu Richard Bukos na Issa Mnally, wamefika mpaka nyumbani kwa marehemu, Kibamba, Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzungumza na ndugu wa marehemu, ambao kwa masikitiko makubwa wanaeleza kuhusu tukio hili, huku msimamo wao ukiwa ni kugomea maiti mpaka sheria itakapofuata mkondo wake.

Leave A Reply