The House of Favourite Newspapers

Afande Sele awaomba msamaha mashabiki zake

AFANDE SELE1Stori: Gladness Mallya, Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Jan 14, 2017

BAADA ya kutangaza kuachana na siasa, mwanamuziki wa Hip Hop, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ ameibuka na kuwaomba msamaha mashabiki zake aliowakwaza kipindi yuko kwenye siasa na sasa alivyojiondoa.

Akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamosi, Afande Sele alisema anawaomba msamaha wote kutokana na kuingia na kutoka kwenye siasa hivyo wamuunge mkono kwenye muziki kwani amerudi rasmi.

“Nawaomba mashabiki zangu wanisamehe, wanipokee kwa mara nyingine kwenye muziki kwani nakuja na kazi mpya nzuri, nguvu zote nimezielekeza kwenye muziki sasa,” alisema Afande Sele.

Hivi karibuni Afande Sele ambaye alikuwa ni mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo pia aligombea ubunge kwenye uchaguzi uliopita, alitangaza kuachana na siasa na kurudi rasmi kwenye muziki.

Wiki Moja Baada ya Ndoa, Masele Chapombe Amtongoza Upya Mke Wake

Comments are closed.