Afariki Baada ya Kudondoka Toka Kwenye Ndege ya Kenya

MTU mmoja ambaye anaaminika ameanguka na kufariki kutoka kwenye ndege iliyokuwa juu ya anga la jiji la London, Uingereza, mwili wake uligunduliwa katika bustani moja katika makazi ya watu juzi (Jumapili).

Mtu huyo ambaye anahisiwa kuwa mzamiaji na akiwa amebeba chakula na nguo, inaaminika alianguka kutoka katika sehemu ya matairi ya ndege ya  Shirika la Ndege la Kenya alikokuwa amejificha, na alianguka muda mfupi kabla ndege hiyo haijatua katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow katika jiji hilo.

Safari ya ndege kutoka Kenya hadi London hutumia saa 8 na dakika 50.

Mwaka 2015, mzamiaji aliyejificha sehemu ya chini ya ndege ya shirika la British Airways iliyokuwa ikitoka Johannesburg, Afrika Kusini, alianguka juu ya paa la nyumba moja wakati ndege hiyo ilipokaribia uwanja wa Heathrow, na mtu mwingine aliyekuwa amejificha sehemu hiyohiyo, alilazwa hospitali kutokana na majeraha.

 


Loading...

Toa comment