The House of Favourite Newspapers
gunners X

AFCON Kundi C: Nigeria Yafuzu, Tanzania Yapata Matumaini Dhidi Ya Tunisia

0

Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025) imeendelea kuwa ya kusisimua, hasa kwenye Kundi C, ambako matokeo ya michezo miwili yaliyochezwa yamebadilisha taswira ya mpambano wa kusaka nafasi za kufuzu.

Nigeria (Super Eagles) waliendeleza mwenendo wao mzuri kwa kuichapa Tunisia mabao 3–2 kwenye pambano lililojaa kasi na ushindani. Nigeria ilionesha umakini mkubwa tangu mwanzo, na juhudi zao zilianza kuzaa matunda dakika ya 44 kupitia Victor Osimhen, aliyefunga bao safi kabla ya kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kiliporejea, Nigeria waliendelea kushambulia na kuongeza bao la pili dakika ya 50 kupitia Wilfred Ndidi, kisha Ademola Lookman akaongeza la tatu dakika ya 67, akionekana kuhitimisha kazi mapema.

Hata hivyo, Tunisia hawakutaka kukubali kipigo kirahisi Talbi alipunguza tofauti dakika ya 74, na baadaye Abdi akafunga kwa penalti dakika ya 87, lakini bado haikuwa enough kubadilisha matokeo.

Matokeo hayo yaliwahakikishia Nigeria pointi tatu muhimu, na kuwaweka kileleni mwa kundi.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Taifa Stars ya Tanzania ilipambana bila woga dhidi ya Uganda Cranes, na kuambulia sare ya 1–1 kwenye dimba la Al Barid, Rabat matokeo ambayo yameacha matumaini bado yapo.

Tanzania ilipata bao dakika ya 54 kupitia penalti ya Simon Happygod Msuva, ambaye kupitia bao hilo ameweka jina lake kwenye historia, akifikisha mabao 25 na kufikia rekodi ya Mrisho Ngassa kama mfungaji bora wa muda wote wa Taifa Stars. Uganda ilisawazisha dakika ya 80 kupitia Ikpeazu, kisha wakapata nafasi ya kuamua mchezo dakika ya 89 kwa penalti  lakini Allan Okello akashindwa kuitumia, na Stars kuondoka na pointi moja ya thamani.

Kwa matokeo hayo, msimamo wa Kundi C unasomeka hivi:

1️⃣ 🇳🇬 Nigeria — 6 pts
2️⃣ 🇹🇳 Tunisia — 3 pts
3️⃣ 🇹🇿 Tanzania — 1 pt
4️⃣ 🇺🇬 Uganda — 1 pt

Leave A Reply