The House of Favourite Newspapers
gunners X

Afghan: Mawasiliano ya Simu Kupatikana Saa 7 kwa Siku

0

Taliban ambao wanaendelea kuiongoza Afghanistan wameweka sheria kali za matumizi ya simu kwa watu wa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambapo huduma ya simu itapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tisa mchana.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Wataliban kujua kuwa simu hutumika kuwapeleleza wanajeshi wake. Hivyo katika kuwalinda wamelazimika kuamrisha kampuni za mawasiliano kutoa huduma kwa muda wa mchana tu.

Wananchi waliomba kuongezewa muda lakini serikali iliwaambia usalama wa wanajeshi ni muhimu zaidi.

Leave A Reply