The House of Favourite Newspapers

Afisa Mkuu wa Fedha wa Anglo Gold Ashanti Atembelea Geita Gold Mining

Afisa Mkuu wa masuala ya fedha (CFO) kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Gillian Doran wiki iliyopita alikaribishwa na kuutembelea mgodi huo uliopo mkoani Geita.

Zulu Nkanyiso, Meneja Mwandamizi wa Mtambo wa uchenjuaji akijibu maswali kutoka kwa Gillian Doran, Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, kuhusu muongozo wa GGML wa usimamizi na uhifadhi wa takasumu (TSF).

Mbali na Doran pia Meneja Mwandamizi wa Ushuru – Afrika, Jacques Labuschagne na Makamu wa Rais wa masuala ya Fedha – Afrika, Himesh Persotam pia waliitembelea GGML.

Ziara yao haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita.

Yusuph Mhando, Meneja Mazingira (aliyeupa mgongo kamera), akimfafanulia CFO wa AngloGold Ashanti Gillian Doran (wa pili kutoka kulia) namna kanuni za mazingira zinazotambuliwa na kufuatwa na GGML katika shughuli zake.

Pia walikuwepo Gilbert Chamlonde, Meneja wa Uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi (kushoto). Kutoka kulia kwenda kushoto: Yusuph Mhando, Meneja Mazingira; Ikingo Gombo, Meneja Mwandamizi – Masuala ya fedha & Mnyororo wa ugavi na Godvictor Lyimo, Meneja Mwandamizi – Utatuzi wa Migogoro ya Kodi.

Mhandisi wa GGML anayedhibiti ubora na viwango vya miradi, Maftah Seif akitoa maelezo zaidi kuhusu teknolojia ya hali ya juu itakayotekelezwa katika kituo kipya cha GGML chenye uhusiano na TANESCO. Mradi huu ni ushahidi wa juhudi za GGML zinazoendelea za kuboresha kuongeza ufanisi wa kiutendaji.