AFRIKA Kusini hadi sasa ina wagonjwa 1,353 wa homa ya Covid-19 ambapo watano wamekufa, kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Afya, Zweli Mkhize ya jana (Jumanne).
Amesema kwamba kifo cha karibuni ni cha mtu kutoka KwaZulu-Natal, ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 46 aliyekuwa pia ana matatizo ya pumu na shinikizo la juu la damu.
Kifo kingine kilichoripotiwa jana ni kutoka Gauteng, cha mzee wa miaka 79 ambaye hakuwa na historia ya kusafiri na ambaye alikuwa Cape Town ambapo alikufa kutokana na matatizo ya mfumo wa kupumua.
Zaidi ya watu 39 000 wamepimwa katika juhudi za kuchunguzwa ugonjwa huo, alisema Mkhize.
Wengine waliokufa ni mwanamke (48) kutoka Western Cape, mzee wa kiume mwenye umri wa miaka 85 kutoka Free-State na mzee mwingine wa kiume (74) kutoka Ladysmith aliyekuwa amesafiri kwenda Mbuga ya Wanyama ya Kruger.