After School Bash yafana Escape One
Msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz akifanya makamuzi yake.Bella 9 akionyesha umahiri wake jukwaani hapo.DJ Zirro (katikati), akisababisha burudani kwenye mashine, chini ya uangalizi wa Adam Mchomvu na B12.Mr Blue na crew yake nzima ya BOB wakifanya yao kwenye tamasha hilo.Nuh Mziwanda akikamua kwa hisia kali.Msamy na madansa wake wakipagawisha jukwaani hapo.Madansa wa Ommy Dimpozi wakiwajibika.Sehemu ya umati wa watu waliyojitokeza kushuhudia makamuzi hayo.
TAMASHA la After School Bash linaloandaliwa na Clouds Media Group kupitia kipindi chake cha redio cha XXL, usiku wa kuamkia leo lilifana vilivyo katika Fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva walifanya makamuzi yao jukwaani.
Tamasha hilo lilikusanya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar, huku wengi wao wakiwa ni vijana wenye umri kati ya miaka 18- 20.
Mmoja wa waratibu wa shoo hiyo Hamisi Mandi ‘B12’, aliwashukuru watu wote waliojitokeza kusapoti shoo hiyo kwani imeweza kuvunja rekodi ya kukusanya watu wengi tofauti na mwaka jana.
“Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza watu wote waliotumia muda wao kuja kujumuika nasi kwenye tamasha hili, kipindi cha XXL, tumekuwa tukiandaa tamasha hili kila mwaka lakini mwaka huu umekuwa wa kihistoria kwetu kwani mashabiki wamejitokeza na wameweza kuburudika kwa amani kubwa kiasi kwamba sikusikia wala kuona aina yoyote ya vurugu humu,” alisema B12.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)