Afumaniwa, ajitosa baharini

Chande abdallah na issa mnally

AIBU! Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zuhura maarufu kama Lolo Princessa ambaye ni mpenzi wa kijana anayejulikana kama Koko Byanco juzikati alijikuta akipata aibu kubwa baada ya kufumaniwa akiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kusababisha mchepuko huo kujitosa baharini katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam kukwepa kipigo.

Tukio hilo lililotokea mchana kweupe na kuwastaajabisha watu, lilitokea jioni ya Oktoba 14 mwaka huu, wakati Watanzania wakiwa mapumzikoni kukumbuka siku ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kilichotokea miaka 16 iliyopita jijini London, Uingereza.

Mapema, dawati la Oparesheni Fichua Maovu (OFM) lilipata taarifa kutoka kwa Koko, akilalamika kuwa amenasa meseji kwenye simu ya mtu wake, ikionyesha mawasiliano na mwanaume mwingine, wakipeana ahadi ya kukutana ufukweni siku hiyo, ambazo zilikuwa na viashiria vyote vya kimahaba.

Koko alidai kwa muda mrefu, mwenzake huyo anayeishi naye Mabibo jijini Dar, alikuwa na tabia ya kuendekeza michepuko bila kujali kuwa wanatarajia kufunga ndoa Novemba mwaka huu na mara kwa mara amekuwa akiwalalamikia mashemeji zake lakini wamekuwa wakimuona muongo.

“Mpaka nimeamua kuja kwenu nataka mnisaidie jamani maisha yangu hayana amani kabisa, naomba mnisaidie nimnase mbaya wangu na hii tabia ikome kwa wote wenye mambo kama hayo. Mbaya zaidi kwao hawajui kama ananisumbua, hivi nataka mashemeji zangu wamuone ndugu yao anachonifanyia,” alisema Koko.

Koko aliwakusanya shemeji zake na OFM ikiongozana na wanausalama, waliondoka kuelekea Coco Beach ambako baada ya msako mkali miongoni mwa mamia ya watu waliokuwa ‘wakila bata’, walifanikiwa kuwaona wawili hao wakiwa wamekaa pembeni peke yao wakiendelea kujinafasi.

Baada ya kuwaona huku makamanda wa OFM wakianza kukusanya ushahidi kwa kupiga picha, mwanaume alishindwa kuvumilia na kuanzisha timbwili kali kwa mgoni wake, ambaye alipoona ‘jeshi’ kubwa likimsogelea, alilazimika kukimbilia ndani ya bahari huku akifukuzwa na mwenye mali.

Baada ya mchepuko kukimbia, Koko alirejea kwa Lolo na kuendeleza mashambulizi, ambayo hata hivyo yalidhibitiwa na mashemeji waliotaka suala hilo kumalizwa kwa mazungumzo. Katika utetezi wake, Lolo alidai aliamua kujifariji ufukweni kwa vile mara nyingi mpenziwe huyo hujifanya yuko bize, hoja ambayo haikukubaliwa kuwa kigezo cha kuchepuka.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Loading...

Toa comment