The House of Favourite Newspapers

Afya ya Rais Lungu Ipo Vizuri

0

RAIS wa Zambia Edgar Lungu amewahakikishia wananchi kwamba yuko vizuri kiafya baada ya kuzimia wakati  akihutubia mkutano wa hadhara, jana jumapili, jijini Lusaka.

 

Katibu wa baraza la mawaziri Simon Miti alitoa taarifa akisema rais ”ni mzima na anaendelea na shughuli zake za kazi”, Dkt Miti anasema Rais Lungu alipata nafuu mara moja baada ya tukio hilo.

 

Rais alikabiliwa na hali kama hiyo ya kiafya mwaka 2015 na wakati huo ofisi yake ilisema kwamba ilitokana tatizo katika umio wake.

 

Rais Lungu anagombea tena uongozi wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika 12 mwezi Agosti.

Leave A Reply