AGGREY & CLIFFORD WAJISHINDIA TUZO YA DHAHABU KUPITIA KAMPENI YA VODACOM
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao amekabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Aggrey & Clifford, Rashid Tenga,Tuzo ya kimataifa ya dhahabu kutoka Spike Asia Festival of Creativity 2017 Nchini Singapore iliyotokana na tangazo lililotengenezwa na kampuni hiyo kwa niaba ya Vodacom kuhusiana na kampeni ya kuuza sehemu ya hisa za kampuni hiyo kwa Umma.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, na imeshuhudia na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.