Agizo la Rais Biden Lazuiwa

Mahakama Kuu nchini Marekani imezuia uamuzi wa Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden wa kutaka iwe ni lazima kwa Watu kuchanjwa chanjo ya Covid 19, kuvaa mask au kupima Corona angalau mara moja kwa Wiki kwenye maeneo ya biashara hususani yanayobeba Watu zaidi ya 100.

Uamuzi wa Mahakama hata hivyo umeunga mkono uamuzi wa Biden wa kufanya iwe lazima kwa Wahudumu wa Afya kwenye Vituo vya Afya na Hospitali kuchanjwa chanjo ya Covid 19.

Rais Joe Biden aliagiza Makampuni na maeneo mengine ya biashara yanayobeba zaidi ya Watu 100 kuchanjwa, kuvaa mask na kupima kila Wiki kwa lengo la kuokoa maisha ya Watu na kuzuia kushuka kwa uchumi kutokana na Covid 19.3470
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment