The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ahofiwa Kufariki Dunia Baada Ya Kufukiwa Na Kifusi 

Mtu Mmoja ahofiwa kufariki baada ya kufukiwa na kifusi wakati akifanya matengenezo katika shimo Mkoani Mara.

Tukio hilo limetokea Agosti, 19,2025, ambapo Mtu huyo aliyetambukika kwa jina la Juma Lutaramula, mkazi wa Katoro Mkoani Geita, ambaye ni fundi aliyekuwa akifanya kazi ya matengenezo ya shimo linalotumika kuchimba dhahabu, katika mgodi wa Kinyambwiga, Walwa Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, ambapo Mtu huyo alifunikwa na kifusi jitihada za utafutaji zikiendelea katika eneo hilo .

Comments are closed.