The House of Favourite Newspapers

Ahukumiwa Jela Miaka Mitano kwa Kuvunja Nyumba na Kuiba Debe la Maharage

0
Nyumba ya Evaristo Mgimba

 

MAHAKAMA ya mwanzo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemhukumu Ombeni Ngwa’vi (25) kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba pamoja na miaka mingine miwili kwa kuiba debe moja la maharage ambapo vifungo hivyo vitaenda kwa kufuatana.

 

Akisomewa shitaka hilo Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu Timoth Mwakisambwe imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya mchana ambapo alivunja nyumba ya Evaristo Mgimba kisha kuiba debe moja la maharage lenye thamani ya shilingi 30,000.

Ombeni Ngwa’vi (25) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba na miaka miwli kwa kuiba debe moja la maharage

Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 294(1)(a), 258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.

Leave A Reply