The House of Favourite Newspapers

Aibu! mke wangu amwaga radhi

0

Na Dustan Shekidele, Morogoro.

MWANAMKE mmoja aliyetambulika kama mke wa mtu, aliyetajwa kwa jina la Mama Sabrana, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta kwenye aibu kubwa, baada ya kufanya mambo ndivyo sivyo ndani ya Ukumbi wa Rose Garden, uliopo Mafiga mjini hapa wakati wa sherehe za kumuaga binti wa dada’ke muigizaji maarufu nchini, Beatrice Holisi ‘Nina’.

Katika pati hiyo iliyoshuhudiwa pia na bondia asiye na mpinzani nchini, Francis Cheka, mmiliki wa kumbi za burudani mjini hapa, Farida Mess Matlou, Afisa Habari wa timu ya Polisi Moro, Mwanaidi Lwena na Afande Janeth kutoka dawati la Jinsia, mke huyo wa mtu aliwakera watu baada ya kuonyesha vitendo visivyo vya kiungwana ukumbini.

Akionekana kama vile amezidiwa na viburudisho, mwanamke huyo alinengua kwa namna ya aibu, kabla ya kuanza kuvua nguo zake, moja baada ya nyingine, kitendo ambacho kiliwakera waalikwa wengine, kiasi cha kutakiwa kutolewa nje.

MC wa shughuli hiyo, Rukia Ndenge ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio na televisheni cha Abood, kwa kushirikiana na Nina, waliwaita mabaunsa ambao walimbeba msobemsobe hadi nje huku waalikwa wengine wakimzomea.

Baada ya sherehe hiyo kumalizika, mwandishi wa habari hizi alifuatwa na watu watatu waliojitambulisha kama ndugu wa mwanamke aliyetolewa, wakisihi kufutwa kwa picha za mke huyo wa mtu, wakidai endapo zitatumika gazetini, zinaweza kuathiri ndoa yake.

“Unajua huyu ni mke wa mtu na mumewe amesafiri, katika hali ya kunusuru ndoa yake, tunaomba ufute hizo picha,” alisema mmoja wa wanandugu hao, akiahidi pia ‘kumpoza’ kwa kiasi kizuri cha fedha endapo atakubaliana nao, jambo ambalo liligonga mwamba.

Leave A Reply