The House of Favourite Newspapers

‘Airport’ ya Istanbul Ndo Kiwanja Kikubwa Zaidi Duniani

UWANJA mpya wa ndege wa Instanbul nchini Uturuki, umezinduliwa rasmi Jumatatu wiki hii, lakini hautafanya kazi kikamilifu hadi mwishoni mwa mwaka huu.   Kwa nini kuzinduliwa kwake kumeharakishwa hivyo?

Ni kwa vile Jumatatu, Oktoba 29, ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya mwaka wa 95 tangu Uturuki kujitangaza kuwa jamhuri.

Uwanja huo wa kuvutia ukikamilika utakuwa na eneo la mita za mraba milioni 76.5.  Unategemewa kuwa uwanja mkubwa zaidi wa ndege duniani uliopo eneo moja na utapitisha abiria zaidi ya 200,000 kila siku.
Uwanja huo uliojengwa kwa utaalam wa kukabili huduma mbalimbali za abiria na ndege, ulishinda zawadi ya kwanza ya mwaka 2016 ya mashindano ya usanifu katika ujenzi yaliyoitwa  World Architectural Festival yaliyofanyika jijini Berlin, Ujerumani.
Gharama ya jumla ya mradi huo ni Dola bilioni 12 (Sh. trilioni 27), na kwa mujibu wa Rais wa Uturuki,  Recep Tayyip Erdogan, uwanja huo utajulikana tu kama “Istanbul Airport.”
Ifikapo Desemba 2018, uwanja mkuu wa ndege wa Uturuki uitwao  Ataturk International Airport, utaacha kufanya kazi na uwanja huo mpya utakuwa ndiyo kituo kikuu cha usafirishaji wa anga katika jiji hilo.
Uwanja huo mpya utachukua nafasi  ya Istanbul Atatürk Airport ambao tayari ni moja ya viwanja 20 vikubwa zaidi vya ndege duniani.

Comments are closed.