The House of Favourite Newspapers

Airtel Fursa Dodoma yawafikia wajasiriamali wadogo wadogo

0

pic 3Meneja uhusiano wa Airtel Jackosn Mmbando akielezea kwa wajasiriamali wadogo wadogo jinsi vijana wanavyoweza kufanya ili kufaidika na mradi wa Airtel Fursa muda mfupi kabla ya kuanja kwa mafunzo yao ya ujasiriamali yaliyodhaminiwa na Airtel Fursa maalum kwa vijana wa Dodoma mwishoni mwa wiki hiii.

pic 1Mwalimu wa ujasiriamali katika semina ya Airtel FURSA Dokta Robert Mashenene ambae pia ni muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE Dodoma akifafanua jambo kwa vijana waliohudhuria semina ya Airtel Fursa mkoani Dodoma kuhusu jinsi kijana anavoweza kukamata fursa na kuzitumia fursa zinazonazomzunguka kuleta maendeleo kwa jamii.

pic 2bBaadhi ya wajasiriamali waliohudhuria mafunzo wakiwa wamemenyoosha mkono kutaka kujibu maswali wakati wa maswali na majibu ulipowadia wakati wa hitimisho la Airtel FURSA

pica 6Mwalimu Chacha Magasi ambaye pia ni mhadhiri kutoka Chuo Cha Biashara cha CBE mkoani Dodoma akiwashauri vijana wasomi na wa elimu ya chini kujiajiri kwa kubuni biashara mbalimbali na kuchangamkia fursa ya Airtel ili kupunguza tatizo idadi ya wahanga wa ukosefu wa ajira hapa nchini

pic 7Mmoja wa vijana Godlove Mato akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiriamali toka kwa meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando, mafunzo hayo yaliandaliwa na mradi wa kuwawesha vijana wa Airtel Fursa mkoni Dodoma mwishoni mwa wiki

pic 4bMmoja wa vijana Godfrey Lymo akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo ya ujasiriamali toka kwa Dokta Robert Mashenene ambae pia ni muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE wakati wa mara baada ya kumaliza kuongoza mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mradi wa kuwawesha vijana wa Airtel Fursa mkoni Dodoma mwishoni mwa wiki

Vijana nchini wametakiwa kuzitumia fursa zilizopo kupitia mpango wa airtel fursa ulioanzishwa na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel wenye lengo la kuwawezesha wajasiriamali kujikwamua kiuchumi na hatimaye kufikia malengo yao kimaendeleo.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika semina ya wajasiriamali wadogowadogo iliyoandaliwa na Airtel mkoani Dodoma kupitia mradi wake wa Airtel Fursa ambapo mwezeshaji wa semina hiyo alikuwa Dokta Robert Mashenene ambae ni mtaalam wa maswala ya ujasiliamaili na masoko na pia ni muadhiri wa chuo cha biashara cha CBE Dodoma.

“vijana wa Tanzania wanapaswa kujituma zaidi kutumia fursa kama zinazowazunguka na kuibuka na mbinu tofauti tofauti kwa lengo la kupata ajira ndani yake na kuendeleza pato la nchi yetu badala ya kulalamikia swala la ukosefu wa ajira mara kwa mara” alisema Mashinene.

Akifundisha somo la ufafanuzi wa jinsi yakusimamia wazo na amewataka watanzania kuachana na fikra potofu za kudhani kwamba watu wanaofanikiwa kupitia kampuni hiyo wanakuwa wameandaliwa na badala yake wachukue hatua ya kushiriki kwa kutuma maombi yao kama inavyoelekezwa.

Kwa upande wake Mwalimu Chacha Magasi ambaye pia ni mhadhiri kutoka Chuo Cha Biashara cha CBE mkoani Dodoma akisaidiana na muwezeshaji huyo anawataka vijana wasomi na wa elimu ya chini kujiajiri kwa kubuni biashara mbalimbali na kuchngamkia fursa ya Airtel ili kupunguza tatizo idadi ya wahanga wa ukosefu wa ajira hapa nchini kwa kuwa Airtel imeamua kuwawezesha na kuwapatia vitendea kazi kupitia fursa.

“Pigeni hodi Airtel ombeni msaada wa fursa ili kukamilisha dhamira ya kusimamia mawazo yenu na kupunguza wimbi la vijana waliokosa ajira” alieleza Mwali Chacha.

Baadhi ya wajasiriamali 220 waliohudhuria mafunzo hayo walisema Semina hiyo imesaidia sana kufungua fikra zao hasa juu ya namna mafunzo hayo yalivyolenga kupanua uwezo wao mwingine wa kujiajiri na sio kusubiria tu.

Nichoraus Sanga alisema mimi nimejifunza kutosubiria tena ajira kuanzia kesho nakomaa na wazo langu la kujiajiri kupitia kilimo cha zabibu na ufugaji wa samaki hapa Dodoma ni bidhaa zinazohitajika sana.

Mradi wa Airtel fursa ni kwaajili ya vijana nchini, Ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo.

Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe [email protected] ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.

Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com

Leave A Reply