The House of Favourite Newspapers

Airtel Fursa msimu huu yawapa wajaliamili milioni 100

0

PICT 1
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (watatu kushoto), akimkabidhi Upendo Litimba, msaada wa vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake vyenye dhamani ya shs milioni 9 kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Mapinduzi , Wilaya ya Nachingwea mjini Lindi. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja masoko wa Airtel wilaya ya Nachingwea Airtel Castle Ngowi akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel Lindi, Edmund Lasway. Anayeshuhudia (kulia) ni mama mlezi wa Upendo Rafii Nachinuku.

PICT 2Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wapili kushoto), akimkabidhi Upendo Litimba, msaada wa ukarabati wa salon na vifaa mbali mbali vya saluni ya wanawake vyenye dhamani ya shs milioni 9 kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Mapinduzi , Wilaya ya Nachingwea mjini Lindi. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja mauzo wa Airtel Lindi, Edmund Lasway. Anayeshuhudia kati ni mama mlezi wa upendo Rafii Nachinuku, akifuatiwa na ndugu wengine wa Upendo.

Airtel Fursa yaingia Nachingwea yampa mjasilaiamali vifaa vya saloon vya mil 9

Ikiwa ni msimu wa pili wa Airtel fursa, jumla ya shilingi milioni 100 za mradi wa kijamii wa Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel tayari zimetumika kwa mgawanyo katika mikoa ya Dar, Morogoro, Dodoma, Kagera Manyara na Lindi

Hayo yamethibitishwa leo na Meneja wa huduma za jamii Airtel Tanzania Bi, Hawa Bayumi wakati akikabidhi saloon pamoja na vifaa vya saloon vyenye thamani ya shilingi million 9 kwa Bi.Upendo Paul Litimba wa mtaa wa Amani katika Kijiji cha Mtua wilaya ya Nachingwea mkoani lindi ambae anaendesha biashara ya saloon.

Bayumi amesema mradi huo unalenga zaidi kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao za maendeleo na zaidi kuleta chachu ya mabadiliko katika Jamii zao.

“Msaada wetu leo kwa Kijana huyu wa hapa nachingwea ni muendelezo wa dhamira yetu ya kuhakikisha tunatumia jumla ya shilingi Bilioni moja tuliyoahidi mwanzoni mwa mwaka huu kwaajili ya kuinua na kuwaezesha vijana katika Jamii zao” alisema Bi Bayumi-

Kwa upande wake Bi.Upendo Litimba ambae ni mjasiliamali wa saaloon ameishukuru kampuni hiyo ya simu ya mkononj ya Airtel kwa kumuwezesha kwa kupatia vifaa vya saloon ikiwemo draya,stiming mshine,genereta, viti pamooja na matengenezo ya saloon hiyo ili kuwa ya kisasa na yenye hadhi ya saloon.

“nitahakikisha nafanya kazi kwa kasi zaidi na pia nitahakikisha nasaidiana na vijana wenzangu kufanya nao kazi ili kujitanua kimapato zaidi, hapa kijijini kwentu Mtua Nachingwea hata kama umeme utakatika bado ninauhakikia wa kuendlea kuhudumia Wateja “ alieleza Bi, Upendo Litimba-Mjasiliamali wa saloon

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa kijiji hicho cha Mtua akiwemo Rose Martin na Janet Malibiche walieleza kuvfurahishwa na msaada huo kwa upendo kwa kuwa sasa wanataokoa muda wanapokwenda kuhudumiwa tofauti na awali ambapo hakukua na vifaa vya kisasa vya kukaushia nywele hivyo kuwalazimu kukaa kwa muda mrefu wakisubiria jua ili nywele zao kuwa tayari kuhudumiwa

Mradi wa Airtel Fursa ni mradi endelevu nchini Tanzania ambapo Airtel imejiwekea malengo ya kuutekeleza ambapo dhamira yake kuhakikisha kila wiki itagusa maisha ya vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 na kuwawezesha katika shughuli zao za ujasiliamali.

Leave A Reply