The House of Favourite Newspapers

Airtel Fursa Msimu wa Pili Wazinduliwa

0

Airtel (1)Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso, akifatiwa na Mshauri wa Airtel Fursa, Eng. George Mulamula kwa pamoja wakionyesha bango kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Airtel Fursa msimu wa pili. Akishuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya.Airtel (2)Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2, mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24 kupata fursa za kuinua biashara zao, uliyozinduliwa Naibu Waziri, Anthony Mavunde katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam.Airtel (3)Naibu Waziri, Anthony Mavunde akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24 kupata fursa za kuinua biashara zao. Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam.Airtel (4)Kijana aliyewezesha kupitia mradi wa Airtel FURSA msimu wa 1, Mohamed Kigumi akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso kwa kufanya vizuri katika biashara yake wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mradi wa Airtel FURSA , mradi wenye lengo la kuwawezesha vijana kufikia malengo yao na kukuza biashara zao. Wakishuhudia (kushoto) ni Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya. (kulia) ni Mshauri wa Airtel Fursa, Eng. George Mulamula.Airtel (5)Mshauri wa Airtel Fursa, Eng. George Mulamula akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili.Airtel (6)Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifatilia uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Saalam.Airtel (7)Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili

* Zaidi ya shilingi billion 1 kusaidia miradi ya kuwawezehsha vijana llings

Dar es Salaam, Alhamis 11th Januari 2016, Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua msimu wa pili wa mradi wake wa kuwawezesha vijana ujulikanao kama “Airtel FURSA” kwa lengo kuendelea kudhihirisha kutimiza dhamira yake kuendeleza huduma za kijamii nchini Mradi wa “Airtel FURSA” ulizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao Msimu wa kwanza wa “Airtel FURSA” umewawezesha vijana zaidi ya 2500 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kupata mafunzo ya biashara na wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea vifaa vilikvyowasaidi kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa zaidi kwa jamii inayowazunguka.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso, alisisistiza dhamira ya kampuni yake kuwawezesha vijana na kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania “Mradi huu wa “Airtel FURSA” unadhihirisha dhamira yetu ya kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao. Msimu wa kwanza wa “Airtel FURSA” umetoa matokeo mazuri sana na tumefanikiwa kugusa maisha ya maelfu ya vijana wengi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini,”

“Katika msimu huu wa pili tunawekeza takribani shilingi billion moja ili kuweza kufikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa na vipaji vyao. Tutaendelea kuwapatia mafunzo ya kibiashara, misaada ya vifaa na kuanzisha mfumo wakisasa wa mafunzo kupitia simu zao za mkononi” alisema Colaso.

Akizindua rasmi mradi wa “Airtel FURSA” Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliwapongeza Airtel kwa kuanzisha na kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ili kuboresha maisha yao, alisema Mh Mavunde “Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali, zikiunganishwa pamoja na fulsa zinazoletwa na miradi kama hii ya “Airtel FURSA” ni wazi vijana wenye malengo Dhahiri ya kujiendeleza wataweza kuboresha maisha yao. Napenda kuwahasa vijana wetu kutumia fursa hii na kufanya kazi kwa bidii:”

“Serikali chini ya Wizara yetu na itaendelea kushirikia Airtel na kufanya kazi kwa pamoja huku ikiweka mazingira bora yatakayochochea vijeza ana kupata fursa ili waweze kuchangia katika kuendeleza uchumi wa nchi” aliongeza Mavunde “Airtel FURSA” ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ili kufikia malengo yao.

Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. Unaweza pia kutuma maombi yako kwa kupitia barua pepe ya [email protected]<mailto:[email protected]>. Or tembelea tovuti yetu ya www.airtel.com<http://www.airtel.com> na ujaze fomu yako ya maombi.

Leave A Reply