The House of Favourite Newspapers

Airtel Fursa, Veta Yawafikia Vijana 18,000 Kusoma Ufundi Stadi Kwa Simu

ARUSHA1BToka kushoto ni Meneja wa Tawi wa Airtel  Ausha Bi Monica Ernest akiwa na Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala Wakizungumza na  baadhi ya wajasiliamali na watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel jana. 

ARUSHA 2Toka kushoto ni  Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala akitoa maelekezo kwa baadhi ya wajasiliamali wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel mkoani jana.

ARUSHA 5Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (katikati) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanaotoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airte jana.

ARUSHA 6

Mkuu wa mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini Bw, Bryton Majwala na wafanyakazi wengine wa Airtel kwa pamoja wakizungumza na  baadhi ya wajasiliamali na watoa huduma ya usafiri wa Boda boda Arusha eneo la stand kuu Arusha jinsi wanavyoweza kujiunga na mfumo wa VSOMO na kusoma masomo ya Ufundi stadi kupitia mtandao wa Airtel jana.

VETA na Airtel kuongeza kozi 10 VSOMO zisomwe kwa simu

Na mwandishi wetu Arusha

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea kutoa uelewa kwa vijana kukamata FURSA na kusomo kozi mbalimbali toka VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO. hadi sasa zaidi ya vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili wanafunzi kuendelea kujisomea.

Hayo yamebainishwa na  Mkuu wa mauzo kanda ya kaskazini  Bw, Brighton Majwala wakati alipoongea na wajasiliamali na madereva bodaboda  waliokusanyika stand kuu  Arusha jana,   

“Airtel na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakiksha mtandao upo vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana zaidi ya milioni 18 wameshakamata FURSA hii kwa kupakua aplikesheni au mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Bw Majwala

Majwala aliendelea kusema kuwa “mpango wetu Airtel na VETA ni  kuongeza uelewa kwa  vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya  ufundi piki piki, umeme wa nyumbani, ufundu simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.

kwa upande wake Meneja  Uhusiano wa Airtel alisema “kutokana na VSOMO kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojisajili  tayari Airtel kwa kushirikiana na wadau wetu VETA tuko katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja na kuongeza  idadi ya wanaosoma na kuhitimu”. alieleza mmbando

“tunampango wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando

 “Mradi wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel FURSA wenye lengo la kuwawezesha vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya  “Airtel the smartphone network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone zao” alisisitiza Mmbando

Airtel kwa kushirikiana na  VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao VSOMO mwezi Julai 2016 ambapo mpaka sasa  tayari mfumo huu umetambulishwa  katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Morogoro na Mwanza lakini kutokana na uhitaji mkubwa kwa  vijana tayari mfumo huo umepokea maombi ya vijana toka mikoa 25  kwa kupakua mfumo/aplikesheni hiyo hiyo na kuomba kusoma kwa njia ya simu za Airtel.

 

 

Comments are closed.