The House of Favourite Newspapers

Airtel fursa yawezesha vijana wajasiriamali Moro

0

Afisa Masoko wa kampuni ya simu mkoa wa Morogoro, Aminata Keita akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya ujasiliamali ya Airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.

Mkufunzi kutoka Veta kanda ya mashariki na kati, Marthin Mollel akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya Airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.

Baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo ya ujasiliamali wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya Airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.

Morogoro, Novemba 1, 2015, vijana zaidi ya 200 mjini Morogoro wamehudhuria warsha ya siku nzima ya ‘Airtel FURSA Tunakuwezesha. Airtel Fursa ni mpango unaowalenga vijana wemye umri kati ya miaka 18 -24 na wanamiliki biashara ndogo ndogo kwa kuwapatia ujuzi na nyenzo muhimu kwa mafanikio ya biashara zao na kuweza kujenga fursa kwa wengine.

Akizungumza katika warsha hiyo, mmoja wa washiriki bw. Musa Ndauka alisema;”napenda kuwashukuru Airtel kwa kutambua changamoto ambazo vijana tunakumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na zana ili kujenga biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua jukumu hili na kutusaidia sisi vijana wa Morogoro”

“Leo hii tumepata stadi za msingi za ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa biashara yangu. Sasa hivi ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti, jinsi ya kutafuta soko la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze kufikia wateja zaidi. Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa maisha yangu. “aliongeza Ndauka

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo afisa masoko wa Airtel Tanzania, Aminata Keita, alisema “tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira. Nchini Tanzania, vijana wapatao milioni moja kila mwaka huwa wanapata matatizo ya ajira. Tunahitaji kuwawezesha na kubadili mawazo ya kutaka kuajiriwa kwa kuwasaidia kuwa wabunifu na kuweza kujiajiri. Mpaka sasa Airtel FURSA Tunakuwezesha imewawezesha vijana zaidi ya 1200 kupitia warsha hii na tuna mpango wa kufikia vijana wapato 2000 mwaka huu peke yake.

Tunatambua na kuwapongeza hawa vijana ambao ni wafanyabiashara wadogo wadogo kwa juhudi walizofanya na kuweza kufikia hapa walipo licha ya changamoto hizi zote. Nami nawahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kuomba kuwezeshwa kupitia mradi wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha”, “alisema Keita.

Alitoa wito kwa vijana katika mkoa wa Morogoro kutumia nafasi hii ya “Airtel FURSA Tunakuwezesha” kwa kuweza kujiendeleza kibiashara na kuhakikisha kuwa wanapanuka kibiashara. Morogoro ina mambo mengi mazuri sana kwahiyo vijana watumie mji wao kuweza kujiendeleza na vile vile kupanua uchumi wa Morogoro. Huu sio muda wa kukaa bila kazi wakati kuna fursa inayokuwezesha kupata maarifa ya bure. Vijana wetu lazima wajishughulishe na vitu tofauti vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali zitakazowafanya wafaidike na kuweza kujikomboa na umasikini, “alisema Keita

Alisisitiza kwamba mpango wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unawalenga wale vijana ambao tayari wanabiashara na walio katika umri kati ya miaka 18-24, na anayeishi Tanzania na kuendesha biashara zake hapa nchini. Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 au barua pepe kwa [email protected] au kutembelea mtandao wa Airtel na kurasa za kijamii kwa maelezo zaidi.

Keita alihitimisha kwa kusema Airtel imedhamiria kufanya kazi na Serikali ili kusaidia kuwajenga vijana na kuwaweka kuweza kuamini kwamba Airtel FURSA Tunakuwezesha’ ipo kwa ajili yao na kuleta mabadiliko na msisimko kwa vijana mkoani Morogoro na maeneo mengine ya hapa nchini.

Leave A Reply