The House of Favourite Newspapers

Airtel Fursa Yazawadia Mil. 7 kwa Mpishi wa Keki

0

PICT 1 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wanne kutoka kushoto), akimkabidhi kijana Diana Mosha, msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala jijini Dar Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa Airtel waliohudhuria hafla hiyo.

PICT 2Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (pili kushoto), akimkabidhi kijana Diana Mosha, msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala jijini Dar Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni (kulia) ni Meneja mauzo wa Airtel Dar Es Salaam ,James Moillo na wafanyakazi wengine wa Airtel.

PICT 3Kijana Diana Mosha (kushoto), akifafanua jambo baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbali mbali vya kutengenezea keki kupitia mpango wa Airtel ‘FURSA Tunakuwezesha’, kwa meneja masoko kanda ya Dar Es Salaam James Moillo (pili kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao Ilala, Dar Es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni meneja masoko wa Airtel kanda ya Mbagala, Saleh Safi akifuatiwa na meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.

 

Dar es Salaam, Jumatano, Januari 27, 2016,

Kufuatia uzinduzi wa hivi karibuni wa Airtel FURSA msimu wa mbili, Airtel inaendelea kugusa maisha ya vijana nchini Tanzania na kuwawezesha kufikia matarajio yao ya ujasiriamali.

Leo Airtel FURSA imemfikia kijana Diana Moshi, mwenye umri wa miaka 22 anayejihusisha na upikaji wa keki jijini Dar Es Salaam. Diana amepokea ruzuku katika mfumo wa vifaa vya kufanyia kazi vikiwemo trei za keki, mashine za kuchanganyia unga wa keki, mashine za kupambia keki, jokofu na jiko la gesi.

Mbali na vifaa hivyo Diana atapokea mafunzo maalum ya ujasiriamali na ushauri wa biashara ya keki kutoka kwa mtaalam maalum na maarufu wa biashara ya keki hapa jijini.

Kutoka alipoanzia akiwa na mtaji mdogo sana wa kuanzia biashara, Diana aliendelea kuwa makini na kutilia mkazo wa ndoto yake. Pamoja na ukosefu wa vifaa Diana hakukata tamaa bali alijifunza kupitia kwa jirani na kukodisha vifaa vya kufanyia kazi kutoka kwa wafanyabiashara wengine.

Akiwa na furaha kubwa alisema; “Niliona Airtel FURSA kama fursa ambayo inaweza kusaidia kupunguza mapambano na kuongeza matumaini yainua biashara yangu, ninashukuru kwamba leo Airtel FURSA imenifikia na kuweza kubadilisha maisha yangu. Nimeanza nikiwa na mtaji mdogo sana lakini leo Airtel imenidhihirishia kwamba kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu inaweza kutimiza ndoto yako “.

Diana aliahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa vile yeye sasa anauwezo kwa kuwa na zana madhubuti za kuzalisha zaidi. “Ninaamini katika kipindi cha muda mfupi nitaweza kuzalisha zaidi na kuajiri wengine ili kusaidia biashara yangu. Mimi ni shuhuda wa kweli kabisa wa walengwa wa Airtel FURSA walioomba na kupata msaada . Ninaahadi kusaidia jamii yangu inayonizunguka kwa sababu ninaelewa fika ni jinsi gani vijana wenzangu wanavyopata tabu huko mtaani na sitaacha kuendelea kuwahamasisha. ”

Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa
Bayumi alimpongeza Diana kwa kufwata ndoto zake na kuhimiza vijana wengine kuiga mfano wa Diana. Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano Bi Bayumi alisema “Diana ametutia nguvu na kuweza kushiriki sehemu ya safari ya ndoto zake kwani ameanza akiwa hana kitu, si kwa mtaji tu lakini hata uzoefu wa kufanya biashara hii. Lakini leo hii ameweza kuuza keki kupitia mitandao na kujipatia hela. Tunaamini vifaa tunavyompatia Diana leo vitabadilisha maisha yake na kuinua biashara yake na kuongeza wateja wengi zaidi.

Tunawahimiza vijana wengi hapa nchini kuchangamkia Airtel FURSA si tu inayotolewa kwa vitendea kazi bali na elimu ya biashara ambayo imekuwa ikitolewa nchi nzima hapa Tanzania, pia kwa kupata maelekezo ya biashara kupitia mitandao yetu ya kijamii inayosadia kuelekeza vijana jinsi ya kukuza biashara zao, kujenga fursa kwa ajili ya wengine na kuwa na huduma na jami zao zinazowazunguka.

Airtel, kwa mara nyingine tena katika mpango wake wa Airtel FURSA umeahidi kuendelea kugusa maisha ya wa Tanzania kwa kuwawezesha vijana kupitia Airtel FURSA. Hadi sasa Airtel imeweza kufikia vijana zaidi ya 2,500 nchini Tanzania na na imeahidi kufikia vijana zaidi ya 1500 katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Leave A Reply