The House of Favourite Newspapers

Airtel kenya yaja na ofa kabambe ya one airtel

0

Nairobi, Oktoba 21, 2015 – KAMPUNI inayoongoza katika mawasiliano ya simu, katika nchi 20 za Afrika na Asia, Airtel, imeboresha huduma yake ya roaming services kwa kuanzisha malipo ya mlingano yenye nafuu kubwa kwa wateja wake wanaosafiri katika bara la Afrika kutokea Kenya.

Huduma hiyo ya ‘One Airtel’ inamwezesha mteja mgeni kutoka nje kutumia SIMkadi yake kupata huduma mbalimbali za Airtel kwa bei ya nchi husika huku akipokea simu bure.

Taarifa ya Airtel, imefafanua kwamba huduma hiyo mpya inatoa bei yenye viwango sawa ndani ya mfumo wa Airtel nchi moja hadi nyingine kwa lengo la kuwafanya wateja kuendea kufurahia kuwa katika familia ya Airtel huku wakipata mawasiliano ya uhakika.

Taarifa hiyo ilisema mathalani, wateja wa Airtel Kenya anayesafiri hadi Madagascar – atafurahisia punguzo la hadi asilimia 85 wakati anapiga simu nchini Kenya kwa kiwango cha shilingi za Kenya 35 kutoka shilingi 227.30 kwa dakika. Mteja wa Airtel Kenya atalipa sh 12 akiwa anapiga simu nchini Madagascar kutoka sh za Kenya 37 kwa dakika. Hii ni tofauti na bei ya soko la Kenya KSh 35 ukipiga simu ndani ya Madagascar na Ksh 285 kwa kupiga simu Kenya ukitokea Madagascar.

Wateja wa Airtel Kenya watakaotembelea nchi 16 zilizo katika mtandao wa Airtel nchini Africa atafurahi huduma hiyo katika mtandao wa Airtel kwa shilingi za Kenya 12 kwa dakika kwa simu ndani ya nchi aliyopo na Ksh 35 kwa kila wito anaoufanya Kenya kutoka nchi hizo au kwa wito wa kimataifa.

Upokeaji wa simu wakati ukiwa katika mfumo wa kususurika utakuwa bure kwa dakika 100 za mwanzo kwenye mwezi

Utumaji wa ujumbe mfupi (SMS) utagharimu shilingi za Kenya 17 ukilinganisha na bei ya soko la sh za Kenya 20 kwa dakika.Ujumbe wa SMS utaingia bure.

Nchi ambazo zipo katika malipo yanayolingana na nchi husika ni pamoja na Nigeria, Zambia, Tanzania, Malawi, Ghana, Sierra Leone, Seychelles, DRC, Gabon, Congo, Niger, Tchad, Burkina Faso na Madagascar.“Airtel Kenya inafurahi kwa mara nyingine tena kuongoza katika kubuni na kutoa huduma bora, zenye nafuu huku tukiwawezesha wateja wetu kuwa huru wakati wanaposafiri katika nchi yoyote ya Afrika iliyo na mfumo wa airtel.

“ Ukiwa na ‘One Airtel’, unaposusurika, maisha yanakuwa rahisi zaidi na nafuu ili kuweza kujiunga na familia, marafiki na wadau wengine. Tumeanzisha huduma hii kuhakikisha kwamba wateja wanaosafiuri wanatumia fursa ya kuwa na mtandao madhubuti wa Airtel barani Afrika kupunguza gharama za mawasiliano,” alisema Ofisa Mtendaji wa Airtel Kenya , Adil El Youssefi.

Uamuzi wa kuwa na huduma hiyo inatokana na wito wa serikali uliotolewa Julai mwaka huu ambapo ilitaka tehama kutumika katika ukuaji wa uchumi kwa kuwezesha mawasiliano nafuu ya kimataifa iwe katika mfumo mmoja au tofauti Wateja wa Airtel wanaolipa awali nao wataendelea kunufaika na huduma ya kulipia gharama za mazungumzo kwa vocha za nchi husika wakati wakisusurika.

Vocha hizo zinapatikana katika duka lolote linalouza vocha za Airtel akwa kupiga “138*jaza namba ya vocha” na kisha bonyeza kitufe cha OK.Huduma ya Kususurika itajipandisha yenyewe mara tu unapoingia katika nchi yoyote yenye mfumo wa Airtel huku kukiwa hakuna haja ya kujisajili upya au kutozwa gharama.

Leave A Reply