The House of Favourite Newspapers

Airtel yabadilisha maisha ya vijana na Airtel Fursa Tunakuwezesha

0

1Kijana Iddy Abdallah Chilumba, akionyesha baadhi ya bidhaa zake anazotengeneza na kuziuza baada ya kuwezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa Tunakuwezesha .Misaada hiyo ikiwemo mashine ya kubangulia korosho, meza maalum kwa kazi hiyo, vifaa mbalimbali na pikipiki mpya inayomrahisishia katika nyanja ya usambazaji wa bidhaa hizo

2Kijana Iddy Abdallah Chilumba, akionyesha baadhi ya bidhaa zake anazotengeneza na kuziuza dukani kwake baada ya kuwezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa Tunakuwezesha .Misaada hiyo ikiwemo mashine ya kubangulia korosho, meza maalum kwa kazi hiyo, vifaa mbalimbali na pikipiki mpya inayomrahisishia katika nyanja ya usambazaji wa bidhaa hizo.

Airtel Tanzania imejikita katika safari ya kuwezesha vijana hapa nchini na kuweza kubadili maisha yao kupitia nyanja ya ujasiriamali kupitia mradi wake wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha”. Ndani ya miezi minne Airtel imeweza kufikia vijana wapatao 1,500 katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa utoaji wa elimu ya ujasiriamali na misaada mbalimbali ya kuwawezesha vijana kwa kufikia ndoto zao kupitia Airtel Fursa. Miongoni mwa vijana hawa ni Iddy Abdallah Chilumba, mmiliki wa biashasra ya korosho ,mwenye mri wa miaka 24 na makazi wa mjini Mtwara.

Iddy alitamani kuendesha biashara ya korosho toka akiwa na umri wa miaka mdogo. Hata hivyo, kama vijana wengi wa Tanzania hakuweza kuwa na mtaji wa kutosha kama moja ya changamoto aliyokabiliana nayo.Akiwa na elimu ya kidato cha nne na stadi za msingi za kompyuta, aliweza kupata kazi ya kuuza duka katika steshenari mkoani Mtwara ili aweze kuisaidia familia yake na kuweza kuhifadhi kiasi kidogo cha fedha na kufanikiwa kuanzisha biashara yake. Kwa mtaji mdogo sana, vitendea kazi duni na ujuzi mdogo katika usindikaji wa korosho, Iddy alijiunga na kikundi cha wanawake waliopata udhamini kutoka SIDO.

Kwa uadilifu wake na misingi bora ya ujana, kundi hilo la wanawake lilimchukua na kufanya nae kazi kama mmoja wao na aliweza kujifunza mambo mengi kutoka katika kikundi hicho. Pamoja na kuwa na mtaji mdogo wa biashara, baada ya muda alianzisha biashara yake mwenyewe. Licha ya kuchukua hatua hii ya kwanza na muhimu kuelekea ndoto yake, Iddy bado alikuwa anakabiliwa na changamoto kubwa kama vifaa vya kufanyia kazi na usafiri wa kusambazia bidhaa zake. Changamoto hizi zilifanya uzalishaji wa bidhaa yake kuwa ya gharama ya juu sana kwani ilibidi kwenda kulipia kwa ajili ya usindikaji na usafirishaji. Ndipo aliposikia Airtel FURSA na kuchangamkia hiyo fursa.

Airtel FURSA Tunakuwezesha imeweza kubadili maisha yangu Iddi alisema”mpaka hapa nilipofikia nimeweza kukumbana na changamoto nyingi. Nilimpoteza baba yangu nikiwa na umri mdogo sana na nikiwa wa kwanza kuzaliwa hivyo kuchukua majujukumu yote ya familia. Hivyo ilinibidi kukatisha masomo yangu na kuanza kusaidia famila yangu. Siku zote nilikuwa na ndoto za kumiliki biashara yangu mwenyewe ya korosho.

Kwa hiyo nikaanza kidogo kidogo na leo hii nawashukuru Airtel kwa kuniona na kuweza kuniwezsha na kuweza kubadili maisha yangu. Kabya ya hapo nilikuwa napata ugumu wa kupata wateja lakini kutokana na Airtel FURSA nimeweza kuongeza mauzo yangu kwa asilimia 55% na usambazaji wa bidhaa zangu umeongezeka kwa hali ya juu sana kwani sina tatizo la usafiri pale ninaposambaza biashara zangu. Vile vile nimeweza kuwapatia vijana wenzangu ajira kwani nimeweza kuajiri watu wawili ambao wanafanya kazi na mimi katika hii biashara yangu. aliongeza, Chillumba.

Airtel inaamini katika kuwezesha vijana ili waweze kujikomboa na umasikini kwa kuweza kujiari wao wenyewe. Kwa kuwatambua na kuwazawadia vijana ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na kuleta mafanikio katika jamii zao. Airtel inatimiza ahadi yake kwa kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao za kujikomboa kiuchumi kwa kujiendeleza wao wenyewe na kuinua wenzao. Airtel inaamini kwmba kwa kumuwezesha kijana katika dunia hii, unamsaidia yeye na jamii inayomzunguka kwa kuleta maendeleo katika jamii hiyo.

Leave A Reply