The House of Favourite Newspapers

Airtel yachezesha droo ya wiki ya 3 ya Promosheni ya Airtel Mkwanjika‏

0

Pic 1Afisa Masoko ya Airtel bi Rebecca Mauma (katika) akibonyeza kitufe cha kutafuta washindi wa droo ya wiki ya tatu ya promosheni ya Airtel Mkwanjika wakati wa kucheza droo hiyo iliyofanyika katika katika ofisi za Airtel Makao makuu morocco jijini Dar es salaam. Wakishuhudia ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bwana Bakari Maggid (kushoto) na Msimamizi wa kipindi cha Tv cha promosheni ya Airtel mkwanjika Abdalah Wambua (kulia)
Pic 2Msimamizi wa kipindi cha Tv cha promosheni ya Airtel mkwanjika Abdalah Wambua (kulia) akiongea mteja wa Airtel mara baada ya namba yake kuibuka kuwa mshindi katika droo ya wiki ya tatu ya Airtel Mkwanjika iliyochezeshwa katika ofisi za Airtel Makao makuu morocco jijini Dar es salaam, chini ya usimamizi wa mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bwana Bakari Maggid (kushoto). Katika ni Afisa Masoko ya Airtel bi Rebecca Mauma

Washindi 28 kutoka katika mikoa mbalimbali wapatikana Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya wiki ya tatu ya promosheni ya Airtel Mkwanjika na kuwapata washindi 28 ambao kila mmoja atapata nafasi ya kuingia kwenye sanduku la pesa la Airtel na kujikusanyia pesa taslimu hadi kiasi cha shilingi milioni moja Promosheni ya Airtel Mkwanjika imekuwa ni promosheni ya kipekee inayowapatia wateja wanne wa Airtel kila siku kuchagulia kupitia droo inayoendeshwa chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nafasi ya kuingia kwenye kisanduku kinachopeperusha pesa na kupewa dakika moja ya kujikusanyia pesa kasha kuondoka na mkwanja wao wa pesa taslimu.

Akiongea na waandishi wa habari, Afisa Uhusuiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema , “mpaka sasa tunao washindi 72 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini kati yao wahsindi 44 wameshajishindia kiasi cha pesa walichoweza kujikusanyia ndani ya sanduku la pesa, hivyo tunajisikia furaha kuwawezesha watanzania na wateje wetu kwa ujumla kuboresha maisha yao kwa kuwapatia kiasi cha pesa kama zawadi ya ushindi wao kupitia promosheni hii ya Airtel Mkwanjika . Washindi 28 tuliowapata leo nao pia watapata nafasi ya kuingia kwenye kisanduchu cha pesa na kujizolea mkwanja hadi kiasi cha shilingi milioni moja.

Akiwataja washindi hao Matinde alisema washindi wa droo ya wiki ya tatu ni pamoja na Issa Salim Kiame kutoka mkoa wa Pwani, Joseph Malingo kutoka Zanzibar, Amina Yusufu mkazi, Hamisi Chande,Ashraf Jumanne, Edwin Mtei, Abdallah Mahambi, Simon Seleman, Abdallah Hamis, Saleh Mohmaed, Derick Shirima,

Salumu Mgwela na Juma Mnende kutoka mkoa wa Dar es salaam wengine ni Erastus Mutachuba na Justine Muganyizi kutoka Bukoba, Manyama Masata kutoka Sengerema Mwanza, George Christian, Mfumbi Vicent, Antony Mluge, Junior Haji kutoka mkoa wa Morogoro, Jessi Mlei mkazi wa Arusha, Bahati Muhawala mkazi wa mkoa wa Mbeya Pamoja na Annastazia Myengwa kutoka mkoa wa Mara Matinde aliongeza kwa kusema ,

ila mteja wa Airtel ana nafasi ya kujishindia, ni rahisi mteja anachotakiwa kufanya ni kununua vocha yake, kukwangu na kuingiza kwenye simu yake au kununua muda wa maongezi kupitia Airtel Money au kununua vifurushi vya Airtel yatosha na namba yake itaingizwa moja kwamoja itaingia kwenye draw ya promosheni ya Airtel Mkwanjika.

“Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu nchi nzima kuendelea kutumia huduma zetu na kuongeza salio ili kupata nafasi ya kuibuka kuwa washindi kupitia promosheni hii ya Airtel Mkwanjika” alisisitiza
Matinde

Leave A Reply