The House of Favourite Newspapers

Airtel Yaendelea Kufungua Fursa Kwa Vijana Hapa Nchini

0

SONY DSC
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi

Kwa Kuendelea kuwapatia mafunzo madhumuti ya biashara.

Katika kupambana na wimbi la kupunguza umaskini hapa nchini, kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unaendelea kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kwa vijana wenye lengo la kuwawezesha na kuwainua vijana hapa nchini .

Mafunzo hayo ya biashara ambayo yamekuwa yakiendeshwa hapa nchini katika mikoa mbali mbali , wiki ijayo yatafanyika Dar Live Mbagala Kuu karibu na Big Bon siku ya Jumanne tarehe 15 ili kuwawezesha vijana kuweza kukabiliana na wimbi hili gumu la kuendesha biashara na kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kuweza kuinua uchumi wa nchi hii.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini, Meneja huduma kwa jamii wa Airtel , bi Hwa Bayumi, alisema “mafunzo haya yanalengo la kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18- 24 ambao wanakiu ya kujikwamua na umasikini. Vile vile “Airtel FURSA Tunakuwezesha” Airtel inawawezesha vijana kwa kuwapatia elimu ya biashara na nyenzo za kuimarisha biashara zao.

Hivyo basi tunapenda kuwakaribisha vijana wote waishio jijini Dar Es Salaam kuweza kuhudhuria mafunzo haya ambayo yatatolewa bure kabisa bila gharama yoyote. Ili kijana aweze kushiriki anatakiwa kufika pale Dar Live siku ya jumanne tarehe 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

Vile vile ili kijana kushiriki au kufaidika na mpango wa Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe [email protected] ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com> aliongeza, Bayumi.

Leave A Reply