The House of Favourite Newspapers

Airtel yaingiza Smartphone ya gharama nafuu Sokoni

Dar-es-Salaam, Jumatano 12, Juni 2019: Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo kwa mara nyingine imeendeleza ushirikiano wake na itel mobile kwa kuzindua simu mpya ya smartphone ya A23 katika hafla iliyofanyika katika duka la huduma kwa wateja la Airtel liliko mlimani City.

 

Kuzindua kwa simu hiyo kunatimiza dhamira ya kampuni ya Airtel kuendelea kukuza utumia na kujikita kuwa mtandao bora wa Startphone yako kwa kuongeza idadi ya watumiaji wa smartphone hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema kuwa Airtel inajivunia kushirikiana na itel kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A23. Kwa kuzingatia kuwa itel imekuwa ikilenga wateja wa kipato cha kati na cha chini, tuliona kuna umuhimu wa kushirikiana nao kwa juhudi hizi kubwa wanazozifanya ili kuhahakikisha kuwa Watanzania wanaishi na kuendana na ulimwengu wa kisasa kwa kutumia mtandao ulio bora na ulioenea kote nchini.

 

Simu ya A23 itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini pamoja na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 36GB chenye muda wa mwaka mmoja ambapo kila mwezi mteja atawekewa na kutumia 3GB.

 

‘Hii simu ya A23 itaanza kupatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kuanzia leo. Zaidi ya hapo, mteja yeyote akatakayeweza kununua simu hii atapata ofa ya kutumia intaneti kwa mwaka mzima bure. Kile atakachotakiwa kufanya ni kuhakikisha ananunua muda wa maongezi wa angalau elfu 1000 kwa mwezi ili kuendelea kufarahia ofa kambambe ya simu hii, alisema Nchunda.

 

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa kutoka itel bw, Eric Mkomoye alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A23 ambayo ina uwezo wa 3G na 4G.

 

Mkomoye alieleza kuwa sifa nyingine za A23 ni ukumbwa wake wa kioo cha inchi 5 pamoja na kamera ya kisasa ya 5mp nyuma na mbele 2mp na inaweza kupiga picha kwa mazingira yeyote yale. A23  inakuja na teknolojia ya kufunga au kufungua  simu kwa sura maarufu kama face unlock Pia simu hiyo ina memory ya 8GB+1GB ambazo zinaweza kuzidi mpaka 32GB.

Comments are closed.