The House of Favourite Newspapers

Airtel Yaja na Huduma ya Tuma na ya Kutolea

Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua huduma  ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money. Huduma hiyo inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea.
…Beatrice akionesha bango lenye ujumbe wa huduma hiyo.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua huduma ‘Tuma na ya Kutolea’ itakuwa ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano (kushoto0 na Mkurugenzi wa Airtel Money  Isack Nchunda wakionyesha bango baada ya kuzindua huduma hiyo ya ‘Tuma na ya Kutolea’. 

 

 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua huduma ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money. Huduma hiyo inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’ itakuwa ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money pale wanapotuma pesa. Huduma ya Tuma na ya Kutolea itawawezesha  wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kujisumbua kukokotoa  gharama ya pesa ya Kutolea.

 

 

 Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda alisema, ‘Tunazindua huduma hii ikiwa ni kuadhimisha yale tuliyoahidi katika wiki ya  huduma kwa wateja ambapo ilianza tangu Oktoba 7 mwaka huu. Airtel imedhamiria kuendelea kuhakikisha ya kwamba inatoa huduma bora muda wote na hii ndiyo sababu tumekuwa tukiwaletea wateja wetu huduma na bidhaa ambazo ni za kiwango cha juu kabisa’.

 

 Kwa muda mrefu, tumekuwa tukiona wateja wa Airtel Money wakituma pesa pamoja na ya ziada ambayo lengo lake ni kufidia gharama za kutolea ambazo ni maarufu kama Tuma na ya Kutolea. Sisi Airtel nia yetu ni kuwapa wateja wetu kilicho bora, leo Airtel imekuja na huduma ambayo ni suluhishi wakati wa kutuma pesa kwani gharama za Kutolea zitakuwa zikikatwa wakati wa kutuma kwa kupitia menu ya Airtel Money. Nia yetu ni kuifanya huduma hii kuwa rahisi, nafuu na ya haraka pale mteja anapofanya miamala yake,’ Nchunda alisema.

 

 

 Airtel imekuwa ikizundua na huduma na bidhaa za kipekee ambazo zinakidhi matakwa ya wateja wetu pamoja na kugusa maisha yao ya kila siku. Tuma na ya Kutolea ni huduma ya kipekee ambayo inawafanya wateja wetu kuendelea kufurahia huduma za Airtel Money, Nchunda aliongeza.

 

Nchunda alisema kuwa huduma hii inapatikana kwa urahisi. Kuanzia sasa, wateja wa Airtel Money hawatakuwa na hofu yoyote kuhusu gharama za kutolea pesa kwani kupitia Tuma na ya Kutolea  huduma ya kutuma pesa sasa imerahisisha kwa kutuma pesa pamoja na ya kutolea.

 

 

Kwa mteja wa Airtel Money kufurahi huduma ya kutuma pamoja ya Kutolea, atatakiwa kufuata maelekezo yafuatavyo;

·         Kupiga menu ya Airtel Money *150*60#

·         Changua 1 Tuma Pesa

·         Changua 3 Tuna na ya Kutolea

·         Changua namba ya Kutuma ya Airtel

·         Ingiza namba ya kutuma

·         Weka kiasi cha kutuma

·         Weka namba yako ya siri

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema, Airtel inatambua kuwa ni muhimu kuweka mahitaji ya wateja wetu mbele. Ni kwa kupitia Airtel Money ambapo mteja anaweza kutuma pesa bure na sasa tumekuja na huduma suluhishi kwenye gharama za Kutolea.

 

 

Tunajivunia kuwa na huduma zenye uwazi ambapo kwa sasa wateja watakuwa na uhakika wa kujua gharama halisi ya kutolea pale wanapotumia huduma ya Tuma na ya Kutolea. Airtel itaendelea kutoa huduma ambazo utapatikanaji wake ni rahisi, nafuu na za haraka ili kukidhi mahitaji ya wateja. 

 

 

Kwa sasa, Airtel inaendelea kuwekeza kwenye mtandao ili uendelee kuwa mpana zaidi na kutoa  huduma za kifedha bora zaidi  hapa nchini. Airtel sasa inajivunia kuwa na zaidi ya 1,000 Airtel Money branches na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 60,000 ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma zote za Airtel kama vile kusajili kwa alama ya vidole, simu mpya za smartphone, vifaa vya simu pamoja huduma nyingine nyingi.

Comments are closed.