The House of Favourite Newspapers

Airtel Yang’aa Maonesho Ya Wadau Wa Mawasiliano Viwanja Vya Bunge Dodoma

0
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akimuelezea Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson kuhusiana na huduma wanazozitoa kutoka Kampuni ya Simu ya mkononi ya Airtel

Kampuni ya Simu ya mkononi ya Airtel leo imeendelea na maonesho ya baadhi ya Huduma na bidhaa wanazotoa ambapo waheshimiwa wabunge na viongozi mbalimbali wamejitokeza kwa lengo la kupata huduma zao.

Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Dkt Tulia Akson aliingoza wabunge wengine leo kupata Huduma kutoka kwa wadau wa Mawasiliano ambapo pia alitembelea banda la Airtel viwanjani hapo.

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alimkaribisha Spika na kumpatia ZAWADI Maalum ya Rauter ya Intanet inayoweza kuunganisha watu zaidi ya 32 kwa Wakati mmoja na Kisha kumweleza mheshimiwa Spika kuwa Airtel inamkabidhi zawadi kwa kuwa inajiamini sasa hata akiwa mkoani (Jimboni) ataunganishwa na Intaneti ye ye Kazi kwa kuwa asilimia 90 ya Minara ya Airtel sasa ya imeunganishwa teknolojia ya 4G ikiwemo Minara ya mbeya.

Maonesho ya wadau wa Mawasiliano yanaendelea kwa siku 3 katika viwanja vya bunge ikiwa ni kuelekea kwenye bunge la bajeti ya Mawasiliano linalotarajiwa kusomwa kesho na Waziri wa Habari na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Mnauye.
Picha Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungwano Tanzania Dkt Tulia Akson Akipokea zawadi ya Router ya Intaneti toka kwa Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando kifaa kinachoweza kuunganisha watu/vifaa Vingine 32 kwa wakati mmoja kwenye mtandao wa Airtel wakiwa mahali pamoja kwa kifaa hicho Kimora. Ni maalum kuunganisha familia, ofisi za wajasiliamali, hotel, marafiki, au kundi lolote lenye uhitaji wa Intaneti ya pamoja.
Leave A Reply