The House of Favourite Newspapers

Washindi wa “Jiongeze na Mshiko” ya Airtrel

0

Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician (kulia) akimzawadia shilingi million moja, Sultan Omary, mfanya biashara anayeishi Dar es Salaam (kushoto), baada ya kuwa mshindi katika droo ya tisa ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”.

Meneja wa Airtel mjini Mtwara, Bartholomew Masatu (kulia) akimzawadia shilingi millioni tatu, Hamis Wed Ally, anayeishi Mtwara (kushoto), baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tisa ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”.

Mfanyabiashara bi. Rachel Nicholas Otaro kutoka Manyara na Mwalimu wa shule ya msingi bw. Hagulwa Mbogo kutoka Dar Es Salaam, Tanzania watangazwa washindi wa droo ya “Jiongeze na Mshiko” inayoendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel.

Nae Sultan Omary, Mfanyabiashara kutoka Dar Es Salaam na fundi magari Hamis Wed Ally kutoka Mtwara walifurahi kuibuka washindi wa droo ya tisa na kuwa miongoni mwa wateja wachache walioshinda katika promosheni hii inayoendeshwa na Airtel.

“Nimefurahi sana kushinda, pesa hii itanisaidia katika kuendesha shughuli zangu na mahitaji yangu ya kila siku. Nawashukuru sana Airtel kwa mapenzi wanaotuonyesha wateja wao kwa kuzindua promosheni kama hii inayosaidia kuinua hali zetu za kiuchumi.

Naahidi kuendelea kushiriki katika promosheni hii na ninamatumaini ya kushinda kiwango cha juu zaidi” alisema Sultan Omary kutoka Dar es Salaam, mshindi wa wiki iliyopita katika droo ya “Jiongeze na Mshiko”.Afisa Mahusiano wa Airtel, Dangio Kaniki alisema kampuni yetu inaongoza nchini kwa kutambua mchango wa wateja wake.

“Kama kampuni inayojali wateja wake, tunapenda kuwazawadia wateja wetu na kuwaonyesha ni jinsi gani Airtel inawajali. Wateja wetu wanastahili huduma bora na wakati wote tunahakikisha tunafikia malengo yao kwa kupitia promosheni ya “Jiongeze na Mshiko” alisema Kaniki Akiongeza “promosheni hii ilizinduliwa ili kuleta msisimko kwa wateja wetu wakati huo huo ikiboresha maisha yao. Tunaamini promosheni hii itasaidia wateja wetu katika kufanikisha mahitaji yao kwa kuwapa nafasi ya kujishindia fedha taslimu”.

Kila wiki unaweza kujishindia milioni 1 au millioni 3. Na mwisho wa promosheni hii mwezi wa 11 mteja mmoja atajishindia fedha taslimu shilingi milioni 50.

 

Leave A Reply