The House of Favourite Newspapers

Airtel yawazawadia wateja wake mamilioni ya “Jiongezee na mshiko”‏

0

Maneja mauzo wa Airtel Kigoma Philip Nkupama (kushoto) akimzawadia shilingi million moja, Bwana Luwi Saulo Karunda kutoka Kigoma baada ya kuwa mshindi katika droo ya nane ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”.

Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician.(kulia)  akimzawadia shilingi million tatu Habibu Mwella Freuzi   (kushoto), shilingi million tatu, baada ya kuwa mshindi katika droo ya nane ya promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”.

Kampuni ya mawasiliano, Airtel Tanzania, imewatangaza washindi wa droo ya tisa ya promosheni ya “Jiongezee na Mshiko” ambao ni, Hamis Wed Ally, dereva wa mabasi kutoka Mtwara, mshindi wa millioni tatu, na Sultan Omary, mfanya biashara anayeishi Dar es Salaam kuwa mshindi wa millioni moja.

Akiongea wakati wa makabidhiano, Afisa Uhusiano na Matukio, Bi Dangio Kaniki, alisema msingi wa promosheni ya “Jiongezee na Mshiko” ni maswali ya maarifa kwa ujumla na inawapatia wateja wake fursa ya kujishindia hadi millioni 50 mwishoni mwa promosheni hii. Hii ni fursa Airtel inawapatia wateja wake kwa kuwapa raha wateja wake na vile vile kuwaongezea vipato vyao.”

“Vile vile Leo tuna furaha kubwa kuwakabidhi washindi wetu wa droo ya nane ya “Jiongeze na Mshiko” ambao ni Kitabu Ally kutoka Kigoma, aliyeshinda Millioni tatu na Habibu Mwella Freuzi , mkazi wa Dar es Salaam, aliyejishindia millioni moja katika promosheni hii ya “Jiongeze na Mshiko”. Hivyo natoa wito kwa wateja wetu kuendelea kushiriki katika promosheni hii ili kujipatia nafasi ya kushinda mamilioni ya fedha.”

“Hadi sasa Airtel imetoa millioni 36 kwa washindi 16 wa promosheni hii kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini. Hii ni ishara ya jinsi gani kampuni yetu ilivyoenea na kuwafikia watanzania wengi hapa nchini.” aliongeza Dangio.

Mmoja wa washindi wa droo ya nane, Bwana Kitabu Ally kutoka Kigoma, aliyeshinda millioni tatu alisema, “Nina furaha kubwa sana kuwa miongoni mwa washindi wa promosheni hii ya “Jiongeze na Mshiko” kwani nilikuwa najaribu mara kwa mara na jitihada hizo zimezaa matunda. Nategemea kutumia fedha hizi kukuza biashara yangu, kutengeneza nyumba yangu na kusaidia familia yangu. Napenda kuwaeleza watanzania wenzangu kwamba promosheni hii ni ya ukweli na wajitokeze kwa wingi na kuweza kushiriki kwani kuna zawadi kubwa ya kushindaniwa mwezi wa kumi na moja.”

 

Leave A Reply