The House of Favourite Newspapers

Aishi Manula afungukia Hatma yake Simba

0
Aishi Manula

KIPA wa Simba, Aishi Manula amebainisha kuwa bado yupo katika kikosi hicho kwa kuwa mkataba wake haujaisha.
Manula yupo nje ya uwanja kwa muda akipambania kurejea kwenye ubora wake baada ya kupata maumivu alipokuwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania.

Taarifa zinaeleza kuwa Manula alikuwa kwenye mpango wa kurejeshwa ndani ya kikosi chake cha zamani Azam FC ili kuendelea kupata changamoto nyigine.

Nyota huyo amesema: “Bado nipo Simba kwa kuwa nina mkataba na timu hiyo. Inajulikana kwamba sijawa uwanjani kwa muda kwa kuwa nilikuwa nimeumia hivyo bado nipo ndani ya Simba.”
Simba itashiriki Kombe la Shirikisho msimu wa 2024/25 baada ya kumaliza ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, GPL

Leave A Reply