Kartra

Aishi Manula Apewa Zoezi Maalum Kumzuia Yacouba

MLINDA mlango namba moja wa Simba, Aishi Manula, juzi Jumanne alikuwa na kibarua kizito mazoezini ambapo alipewa mazoezi magumu kwa muda wa saa moja, akiandaliwa kuzuia hatari zote za washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Yacouba Songne.

 

Simba na Yanga zitakutana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, huku Yanga wakijivunia mshambuliaji wao Yacouba aliye kwenye fomu ambapo mpaka sasa amehusika kwenye mabao 10 akifunga sita na kuasisti mara nne.

 

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Dar na kushuhudiwa na Spoti Xtra, makipa wote wa Simba, Ally Salim, Beno Kakolanya na Manula walifanya kwa dakika 45, kisha Manula akapewa program maalum ya dakika 15 peke yake.

 

Chini ya Kocha wa Makipa wa Simba, Milton Nienov raia wa Brazil, Manula alipigiwa mashuti makali 11, ambayo aliyaokoa kwa ustadi mkubwa jambo lililoonesha wazi kwamba yupo fiti kuzuia hatari za Yanga.

Stori: Musa Mateja, Joel Thomas na Hawa Aboubakhari


Toa comment