AISHI NA MAITI YA MAMA YAKE KWA AJILI YA PENSHENI

MTU mmoja nchini Hispania anayedaiwa aliishi na maiti ya mama yake kwa mwaka mzima akiwa ameificha ili aendelee kupata pensheni aliyokuwa anaipata mama yake, amekamatwa na polisi jana (Alhamisi).

Polisi waliugundua mwili wa mwanamke huyo uliokuwa umeharibika vibaya katika fleti moja jijini Madrid siku ya Jumatano baada ya kujulishwa na majirani kutokana na harufu ya ajabu iliyokuwa imeenea sehemu hiyo.

Polisi walimtia nguvuni mtoto wa mwanamke huyo ambaye ana umri wa miaka 62 kutokana na udaganyifu na kushindwa kuripoti kifo cha mama yake aliyekufa akiwa na umri wa miaka 92 huku akiendelea kuchukua pensheni yake.

 

Loading...

Toa comment