“Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi ambaye aliovertake pasipo kuchukua tahadhari na kukutana na gari nyingine mbele kisha ajali ikatokea, dereva wa basi ametoweka na tunamtafuta, kama hatopatikana tutamkamata mmiliki wa basi ili atuoneshe dereva alipo”. Amesema Mutafungwa.
Jeshi la Polisi limethibitisha kwamba: “Ni kweli usiku wa kuamkia leo Ijumaa Agosti 16, 2019, majira ya saa 7:30, kumetokea ajali eneo la Nanenane, basi mali ya Safari Njema likitokea Dar kwenda Dodoma limegongana kwa ubavu na lori mali ya Tumbaku Alliance, watu wanne wamefariki akiwemo dereva wa lori.”
Comments are closed.