
SHIRIKA la ndege la United Airlines la Marekani limesema linasitisha safari za ndege zake 24 aina ya Boeing 777 baada ya moja ya ndege hizo kupata hitilafu ya injini baada ya kuruka siku ya Jumamosi.
Ndege hiyo ya Boeing 777, iliyokuwa na abiria 231 na wafanyakazi 10, ilifanikiwa kutua salama katika uwanja wa ndege wa Denver. Hakuna majeruhi walioripotiwa. Mabaki ya ndege hiyo yalionekana yamesambaa karibu na makazi ya watu.
Ikizungumzia tukio hilo, Japan imeyataka mashirika yote yanayotumia za Boeing 777 zenye injini za Pratt & Whitney 4000 kuepuka kuruka.
Boeing imesema inaunga mkono uamuzi wa Japan na imependekeza kusimama kwa shughuli zote za Boeing 777 zanye injini kama hiyo wakati uchunguzi kuhusu tukio hilo ukiendelea. Watengenezaji wa aina hiyo ya ndege wamesema ndege 69 za Boeing 777 ziko kwenye matengenezo kote duniani zenye injini ya aina hiyo.
Ndege ya shirika la United namba 328, iliyokuwa ikielekea Honolulu ilipata hitilafu kwenye injini yake ya kulia, Mamlaka ya anga (FAA) imeeleza. Shirika limetaka uchunguzi zaidi kufanyika kwa aina ya ndege ya Boeing 777 zenye injini za Pratt & Whitney 4000 baada ya ajali hiyo.
‘Ilikuwa ikitikisika hasa…’ Mmoja wa abiria aliyekuwa ndani ya ndege hiyo ameliambia shirika la habari la AP kwamba rubani alikuwa akitoa tangazo wakati mlipuko mkubwa ulisikika.

